Mkwasa umeteleza kaka na usirudia tena wakati mwingine

py thon

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2016
Posts
2,476
Reaction score
4,448
Leo Mwasa kaitisha press na kulizungumzia sakata la Mchezaji wa Azam Gadiel Michael na Yanga kuna kauli Mkwasa kasema ni rahisi kwa mchezaji wa Azam kwenda simba kuliko yanga.

1.Mkwasa naomba nikukumbushe ndugu yangu huenda uliteleza umesema takriban wachezaji 4 wametoka Azam na kwenda simba bila shida yeyote ila nataka nikukumbushe Mkwasa wachezaji waliosajiliwa simba kutoka Azam ni makombo "wachezaji waliotemwa kikosini" mfano ni Bocco alitemwa na alikuwa mchezaji huru hivyo ilikuwa ni choice yake aende wapi pia kwa kesi ya Manula na Kapombe ni hivyo hivyo walitemwa.

2.Lakini kwa kesi ya Gadiel Michael ni tofauti Azam wanamhitaji bado sababu ya umri wake mdogo na kiwango na pia yupo ndani ya mkataba.Lakini mchezaji ameonyesha nia ya kuondoka anashindikiza kuondoka sasa hapa mlipaswa mkae meza moja na Azam na mlipe ada ya uhamisho Lakini wewe Mkwasa ulifanya ndivyo sivyo mlimsainisha Gadiel ambaye yupo kwenye mkataba na Azam bila ya waajiri wake kujua yani hapa mngekuwa ulaya basi klabu na mchezaji wote mngepewa adhabu kali sana .juzi nilikuwa namsikiliza Gadiel Michael akihojiwa efm alilalamika sana na kulia lia sana kuwa Azam wanamfanyia mtima nyongo lakini Gadiel unafahamu fika upo ndani ya mkataba kwanini usaini yanga bila ya Azam kujua au bila ya Azam na yanga kuongea ?

Twende ulaya kidogo nadhani sote tumeshuhudia saga ya Neymar aliyekuwa anataka kwenda Psg lakini alikuwa ndani ya mkataba na Barca na siku ya kuripoti kambini aliripoti na kufanya mazoezi na kucheza michezo ya pre season huku akifuatilia uhamisho wake na kusubiria PSG na Barca wakubaliane na walipe ada ya uhamisho 222M ili auvunje mkataba aende PSG baada ya PSG kulipa 222M Neymar alienda kujiunga na kusaini mkataba wake PSG

Lakini ndugu yangu Gadiel kinyemela umeenda kusaini yanga ilhali una mkataba Azam halafu unaanza kulia lia unawekewa mtima Nyonga

Na Mkwasa umeteleza kusema tumemsainisha Gadiel ila tulivyotajiwa bei tumeshindwa
Leo hii klabu ya Morocco imetoa kitita cha 120,000 kumsainisha Msuva aliyekuwa kwenye mkataba yanga na nyie toeni pesa kwa Azam mvunje mkataba ,kesi ya akina Bocco walikuwa wachezaji huru .



Gadiel juzi nilimuonea huruma alivyokuwa analalamika ila kwasasa inabidi uwe mpole na Mkwasa utamsainishaje mchezaji bila ya kufuatilia kwa kina
 


Hao ndiyo viongozi wa mpira Tanzania, hawajuwi chochote.
 
Pre-contract siyo kinyemela nikawaida tu ktk soccer baada ya miezi 4 atakuwa huru nakuondoka sasa umri mdogo utakuwa umewanufaishaje Azam!!?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo ni pre contract wewe, hiyo ni kawaida timu nyingi huwa wanafanya hivyo
 
Issue ndogo hivyo umekuja na gazeti lote hili
Usiangalie tu sababu ya Mkwasa anakuhusu, ndiyo uwone issue ndogo, hawa akina mkwasa ndiyo viongozi wetu wa mpira, leo yupo Yanga kesho TFF, leo anachanganya mambo hivi alafu tukapiga mskofi kumshangilia, kesho akiwa TFF hutoweza kumtofautisha na Malinzi.
 
Ni rahisi kupitia uzi wa mleta hoja hapa jukwaani na kubashiri kiwango chake cha ueledi au nafasi darasani aliyokuwa anashika,mleta uzi kama huyu unapitia hoja zake na kuishia kutikisa kichwa yaani SIFURI kabisa...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
POVU LINAKUTOKA UNGEKUWA YANGA SI SHIDEE
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…