Mkwasi Rostam na Vodacom



Ni kweli, una haki ya kujadili hata kama unatofautiana na wengine.
Ila nilitegemea tayari ungekuwa umeshapata majibu ya maswali yako kwa kusoma post za waliokutangulia.


.
 
Mnaonaje kama tutasusia kutumia noti zenye signature ya Ballali kwa kuwa ni fisadi... how does that sound..
 
Masatu----Inakuja sasa kila product ya kampuni tutazigomeaa.....sijui ngoja tuone....wadau hili la Noti je?Vipi umeme wa Dowans unaiongia kwenye Gridi ya Taifa?ni mawazo tu...Lunyungu je?upo?
 
Mnaonaje kama tutasusia kutumia noti zenye signature ya Ballali kwa kuwa ni fisadi... how does that sound..
Hili linawezekana huko Pemba... Sijui Bara kama wana ubavu huo...😀 😀
 
Hii hoja ni muhimu sana, na ninauhakiwa wataalam wa uchumi wa Voda kama wako serious angalau wameshtuka kidogo na kisha itakuwa angalau AOB katika moja ya vikao vyao, napenda kuwakumbusha VODA kuwa Mwanzo wa hesabu ni moja na wasipuuzie hii mada, mwisho ni kweli kuwa Kama uongozi wetu wa nchi hauchukui hatua kwa watu kama RA hii ni njia mwafaka kabisa ya kuwashughulika mafisadi. Naunga mkono hoja hii kwa kuwa naamini uongozi wa Voda hautakubali kuona shirika lao linachafuliwa kwa kumkumbatia Rostam, watamtupilia mbali.
 
Alafu wakuu swala la ajira pale VODA nasikia ni za kimanyagu nyagu yaani unaajiliwa kama kibarua kwani baada ya miezi kama 6 hivi wanakutemesha tena.Nilimsikia jamaa mmoja analilalamikia hilo.Kwa hiyo kwa mtindo huu hili kampuni halisaidii walalahoi kwani linaneemesha watoto wa vigogo tu wenye kupewa shavu na mishahara minono si mnamwona binti wa MAKAMBA kakalia kitengo pale VODA kuna watoto wa vigogo wengine wapo pale.Tunaomba mwenye full data amwage hapa hata nyie mliopo VODA hapo mwageni news hapa tunawasaidia wenyewe msifanye mzaha mwageni ukweli humu ndani JF.
 
Vp kuhusu ushabiki wa mpira ligi kuu inadhaminiwa na VODACOM, mashindano ya MA-MISS wa kibongo nayo wanadhaminiwa na VODACOM sasa sie tunaweza kujitoa wote na je tulio wapenzi wa mpira tutawashawishi vp kina Simba,Yanga,Prison,Mtibwa na wengineo wakatae udhamini wa VODACOM kwa sababu ya huyu RA wakati ndio wanawaweka hapa mjini.
Inabidi tuanzie kwenye mzizi mkubwa kuukata ndipo tufuate matawi, ukikata matawi baada ya muda mengine yatachanuwa cha msingi ni kuanza kukata huu mzizi mkubwa unaofanya mti unakuwa na kushamiri kila kukicha na unatoa kivuli kizuri.
 
Mnaonaje kama tutasusia kutumia noti zenye signature ya Ballali kwa kuwa ni fisadi... how does that sound..

Masatu it is has been long time , you were gone , hii comment si yako nakujua you are smart kutoa mfano wa aina hii .Masatu kama utasoma hapa angalia tena password yako ama badili .Huyu si wewe .Kwamba unalinganisha nma kampuni inayo tula na kuchangia pato la fisadi ambaye hawezi kukamatwa wala kuguswa na sahihi ya Marehemu Balali kuwa kwenye noti yetu tuisusie ? Nisusie noti ya Tanzania nitumie ya Nchi gani ? Nimelata hoja mbele yenu kwa sababu ya uzalendo kwa Nchi yangu kwamba vita ni kali na tuanzie kila kona maana si CCM wala Serikali wako tayari , tena nisusie noti ya Tanzania ? Jamani inakuingia akilini ? Hii ni sahihi ambayo soon itakuwa imeanza kutumika ya Ndullu , sahihi ya Balali haipeleki pesa wala utajiri kwake kila tukitumia noti le Vodacom wanaingiza pesa na kutuona wajinga na wapayukaji tu maana wanatula kwa kila hali .

Nasema kampuni ama bidhaa yeote yenye mkono wa Fisadi kama tunaweza kuiepuka tufanye hivyo kwa nguvu zetu zote .
 


Kwanza nakupongeza Lunyungu kwa wazo zuri sana. Pia ndugu yangu Masanja maelezo yako ni safii ili kuweka sawa pointi hii. Mahatma Gandhi alipitisha kampeni kugomea chumvi ya Waingereza na akawahamasisha wananchi kwenda baharini kutengeneza chumvi ya bure. Alifanya hivyo kwa kuwa aliamini pesa iliyopatikana kutoka kwa wahindi kwa kununua chumvi iliyotengenezwa katika viwanda vya Waingereza, ndo ilitumika kugharamia ukandamizaji India. Waingereza walisalimu amri.
Mimi tangu 2002 situmii Vodakom sikuipenda tu. Wazazi na ndugu zangu baadhi wanatumia Voda lakini nimekuwa nikiwashawishi kuachana nayo kutokana na kutokuwa na mapenzi nayo,lakini sasa nimepata sababu ya Msingi ya kushinikiza mabadiliko hayo.
Jeuri ya RA ni pesa na hatuwezi kuendelea kumuongezea nguvu hiyo hata kama ni pesa kidogo. Watanzania tufungue macho, pale tunapopata nafasi ya kupambana na hawa watu tuitumie ipasavyo. Tusibaki kulalamika tu. Let us play our part.
 

Huyu bwana nadhani ana shea tu huko Voda, hivyo wakianza kuona mauzo yanadorora nadhani itabidi wamteme RA na kumuomba auze shea zake na atoke ndani ya Voda.
Ni kweli kuwa kuna baadhi ya Watanzania ambao wameajiriwa na Voda, lakili huyu RA anaathiri Watanzania almost wote, hao walioajiriwa ni kaasilimia kadogo sana.Hivyo hatuwezi kuwaweka wao mbele.
 
Kudos Lunyungu kwa wazo zuri...........JF oyeee

......Lunyungu unajua wazo kama lako nililishuhudia kwa Mwanangu kutupa ktk garbage bin audio CD za South Africa.....ikiwa ni kuonyesha hakubaliani na vitendo wanavyowafanyia ndugu zetu huko SA

......hili ni wazo zuri sana na tulitumie kwa mafisadi wengine pia
 

Borntown nimekusoma na kukuelewa ial kwa sasa fanya lile unaloweza .Mengine makubwa kwa kuwa yanahitaji ushawishi mkubwa ambao bado hatuna kwa hao ulio wataja basi sisi tufanye hili ambalo tunaweza .Slowly message itaenea na wachukia ufisaidi wote wataamua kutuunga mkono.
 


Naunga mkono hoja, maana nadhani TZ ni miongoni mwa nchi chahce zeny mitandao mingi ya simu za mkono.

Mimi VODA nilijitoa siku nyingi na nataka kuongeza line nyingine lakini si VODA.
 
Mnaonaje kama tutasusia kutumia noti zenye signature ya Ballali kwa kuwa ni fisadi... how does that sound..

Mkuu Masatu naona hapo umeteleza kidogo!
Tukisusia noti zenye saini ya Balali maana yake hatutauza wala kununua na hivyo hatutakula! Sasa tukiwasusia Vodacom hatutawasiliana?

Rudi ndani ya mada, tafadhali
 
Mkuu Masatu naona hapo umeteleza kidogo!
Tukisusia noti zenye saini ya Balali maana yake hatutauza wala kununua na hivyo hatutakula! Sasa tukiwasusia Vodacom hatutawasiliana?

Rudi ndani ya mada, tafadhali

Kama alivyosema Ibrah, Masatu hapa umeteleza kidogo. Noti hizi sio mradi wa Balali au mali yake. Hakuna anachogain kwa sisi kuwa na noti za Tanzania zenye saini yake. Huu mfano hauingii hapa.
 
Wewe Lunyungu sasa unaishiwa, yaani watu wasitumie vodacom au bidhaa za Rostam Azizi kisha watatumia nini? Rostam amekukosea nini mpaka ukatae kutumia bidhaa zake?

wakati mwingine natamani ungekutana na Hitller uso kwa uso enzi za uhai wake halafu umwambie kuwa "wayahudi" ni watu safi uone kingetokea nini!
 
No no no hapo bado hauja tushawishi tuache kutumia mtandao wa Voda kisa ni wa RA tena kwa hiyo mada yako isiyokuwa na ushahidi wowote. Please kama una ushahidi wa uhakika uweke hapa kila mtu aone. La sivyo hadi house girl wangu naenda kumnunulia line ya VODA. siwezi kushawishika kwa hayo maneno yako tu.
 

Bravo Lunyungu
Hii ni njia moja nzuri ya kuonesha kuwa haturidhishwi na huyu mtu. Ni lazima tuchukue hatua i think it is wise if we get the message sent. Lazima tuoneshe uzalendo kwa taifa letu. Wanaomtetea RA wana lao
 

Unataka ushahidi wa aina gani ? Umesoma hata mtu katoa hapa jedwali kuonyesha Rostam ana share ngapi kule Vodacom ? Ina maana ni kwlei hujui kwamba RA ana share vodacom ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…