Mkwasi Rostam na Vodacom

tiGO for life....

Jamani kwa nini mnaumiza vichwa na kupigizana kelele na watu ambao kwa namna moja au nyingine wanausika na hao watuhumiwa wa ufisadi??

Mimi niwaambie kitu kimoja.. hao wote wanaong'ang'ania kutumia voda ni mafisadi kwa namna moja au nyingine.. Kwa nini nasema hivi...
Hebu ajitokeze mtu mwenye ushahidi hapa Jf kama kuna kampuni yoyote ya simu yenye viwango vilivyo juu kama VODACOM, utume msg utakatwa pesa nyingi upige simu utakatwa pesa nyingi yaani ni kufilisiana kwa kwenda mbele hakuna kingine zaidi ya kuchuma pesa ya mvuja jasho kiulainii alafu mnaenda kudanganya walalahoi kwa udhamini wenu feki ambao hata pesa ya kumsajili kaseja imepita huo udhamini wenu si aibu hiyo??

Naungana na mkuu LUNYUNGU kuwasihi woote mnaotumia VODA ni vyema mkaachana na hiyo kampuni maana ni wanyonyaji wakubwa..... lasivyo tutabakia kusema kama ningejua ningesikiliza ushauri wana wana JF ....

Kumbuka LIFE IS A FULL OF IF
 
Sawa, hata hivyo, lengo kubwa kuliko yote sio kumkomoa mtu hapa bali ni kutokomeza ufisadi kwa njia tunazoweza kutumia ikiwemo hii ya kususia.

Hili la kususia nimeliona ni muafaka sana kwamba tutaweza kumshawishi hata mwananchi aliyeko kijijini akashiriki kwenye hili na yeye kutambua kwamba kumbe anayo silaha ya kupambana na wahujumu wa nchi ya mababu zake (maana sidhani sasa tunapozungumza nchi hii ni yetu tena).

Hali kadhalika yeye kuona matokeo ya kususia huku - right then. Njia hii naiona ina ufanisi zaidi ukilinganisha na jitihada za kumuelimisha mwananchi kuhusu uwezo wake au nguvu aliyonayo kwenye kupiga kura!

We want our voices to be heard! Hata kama RA ataendelea kuwa tajiri, that is irrelevant to me, there is one thing I want to put a STOP to it na si kingine bali ni UFISADI.

Je ungetaka kumshawishi babako ashiriki maandamano japo kuna police na wana live bullets ungali ukifahamu kwamba njia mbadala zipo? Kwanini basi tushindwe kuwashirikisha wananchi vijijini bila kuwatumbukiza kwenye risks kubwa wakati we have the means? Ni wengi wanatambua dhuluma wanayofanyiwa isipokuwa tu hawajui namna wanavyoweza kushiriki kuikomboa nchi hii toka kwenye mikono ya akina RA.

Tutizame outcome ya hili moja kwanza. Ukihamia Celtel (suppose nako kuna MIFISADI) hakika watatia maji wakiona VODA ananyolewa.

Nakubaliana nanyi kwamba hili lina IMPACT kubwa sana.




.
 
Nimesoma maoni ya wengi na bado naitisha mgomo.Mimi nililenga kisiasa kumbe hata gharama zao ni kubwa nalo limeongezea hili .So tuendelee kupiga makelele ya mwizi hadi kieleweke .

Nina wapa pole wageni 2 ambao wamelazimika kuingia kumjibia RAna Vodacom yao .Uchumi wa Nchi una faida gani kwa Baba na Mama yangu kijijini kwetu ?Hakuna kabisa .Kama siwezi kujitahidi kuwaoa pesa ya kula basi hawawezi maisha na wazee sana .Faida wanaziona mafisadi na si mimi na watu wa kijiji kwetu .
Nawaone huruma kwamba mnakuja wakati mambo ni moto sasa .Tutazidi kuelezana hadi kieleweke tu hapa .Hatuwezi kuungana na CCM kwa kushindwa kuwawajibisha wezi no .Lazima kutafuta silaha ya kupambana nao tu .

Mawazo ya kifisadi haya toka shy na ndugu hawa wapya ambao naamini wametumwa kuja ku spin ni sawa na akili ya Chenge kwenda kumwaga unga kwenye viti vya wabunge anao wachukia Dodoma.

As for Shy .Uongo mwingine hauna maana hata mara moja .Mimi nawe tumewahi kuongea wakati ule wa issue Muhimbili na tokea nilijue you were a senior snitch .Sina mawasiliano nawe hata siku moja na hili linathibitisha madai ya wengi hapa natabia zako .Mimi kuwa Kongo ?Nafanya nini ? Nilete kwako computer ? Yaani kwa akili yako unadhani mtu mjanja kama naweza kuja kwako kuleta computer etu utengeneze ? Kama akili yako kwa hapa ni kama unyoa bado kweli mimi nikae chini nikutafute wewe ? Chekesha umma mimi simo,

Narudia wito wa kuanza na Rostam na Vodacom kwanza .Hili ndilo muhimu kwa sisi hapa .Tuonyeshe kuwa serious kila tukiongea na si maneno .Time now to ditch Vodacom pamoja na kwamba ndugu zetu wana ajira huko .
 
KAKA HAWA JAMAA MASIKIO YAO HAYASIKII NA MACHO YAO HAYAONI TENA,ATA UKIWAFINDISHA HAPA KAMWE HAWATAELEWA.WANAOTA TU HAPA HAKUNA MWENYE UJANJA WA KUWAZUIA VODA KUPETA
 
VIWANDA GANI VYA NGOZI AMBAVYO RA ALIVIFILISI????HAYA NI MAJUNGU MAKUBWA.UNAPOSEMA ALIPEWA KANDARASI ZA SERIKALI LAZIMA UZITAJE NA SIO KUGENERALIZE...MIMI NAKUBALIANA NA HUYO NCHIMBI KUWA WAKATI VODA INAANZISHWA HAKUNA UFISADI WOWOTE AMBAO UNATAJWA WA EPE WALA RICHMOND SASA KUSEMA KUWA VODA INATOKANA NA HIVYO NI MAJUNGU MAKUBWA SANA SANA.HATA KAMPUNI YA KAGODA KAMA KWELI NI YAKE HAIKUCHUKUA FEDHA MIAKA HIO YA 1999 MPAKA 2000 VODA IWE TAYARI KUANZISHWA.WIVU WA KIKE TU UMEKUJAA
 

Naona Mkuu umewasha moto kweli kweli inatakiwa kama watu wako makini wachukue hatua haraka mpaka Vodacom wahakikishe wanamtimua FISADI.
 
Namshukuru Mungu hizi pesa zilichukuliwa na mtu mwenye akili kama RA kwakuwa ingekuwa ni sisi waswahili ungekuta tayari tumeongeza wake tu hapa....kwanza kama ni kweli alichukua ni sawa na naita ni wizi endelevu kwa kuwa ameiba pesa ambayo imekaa tu bot,amewekeza na amewapatia watanzania ajira,watanzania zaidi ya elfu moja wamepata ajira voda.mwananchi na zaidi ya wananchi elfu tatu wana ajira caspian..Mungu akuzidishie ndugu yangu Rostam Rasul Abdul Aziz....
 
LUNYUNGU hebu tupatie vielelezo ili tukuunge mkono maana zisiwe habari za mitaani au labda una chuki binafsi na huyo Rostam
 
LUNYUNGU hebu tupatie vielelezo ili tukuunge mkono maana zisiwe habari za mitaani au labda una chuki binafsi na huyo Rostam

Ipole
Unataka vielelezo gani ? Unataa ushahidi juu ya RA kuwa na share vodacom ? Au ni kitu gani huelewi mkuu ?
 

Ama kweli akili ni nywele .Kama RA anaweza kulala mbele na mapesa ya EPA , huko nyuma tutamwamini vipi kwamba alitumia pesa zake kunuua hisa Vodacom? Hapa issue ni kwamba ni Fisadi leo na kama ana kitu alikuwa nacho kabla hajajulikana kwamba ni Fisadi na leo kajulikana lazima alipe price .Hii ndiyo maana ya sisi kuitisha mgomo na kumwaga somo watu waachane na Vodacom
 
Ipole
Unataka vielelezo gani ? Unataa ushahidi juu ya RA kuwa na share vodacom ? Au ni kitu gani huelewi mkuu ?
MIMI NATAKA VYA KUWA WAKATI VODA INAANZISHWA NI PESA GANI ZILIIBIWA NA UFISADI NA WAPI?NA ANA SHARE KIASI GANMI ILI KUJUA KAMA KWELI NA ZA HUO UFISADI WAKO UNAOSEMA
 
 

Nakubali wazo lako moja kwa moja. Ila nakataa kuwa RA na wenzie hawagusiki!! Mbona mimi nauona mwisho wao!!! Cha msingi kila mtu afanye awezalo kuwaangusha!

Mapambano yanaendelea
 
Ususiaji wa bidhaa za kifisadi ni jambo common sana duniani kote si kenya tu! Hata wazungu (wanaharakati) wakisikia kuna blood diamonds na bidhaa kama hizi wanazisusia! Afterall hawa voda ni ghali
 
Mh Lunyungu umenichekesha kweli angalau na wewe umeliona hilo....nikisema mimi huwa napuuziwa lkni maadamu na wewe umeliona hilo labda mambo yatabadilika kadiri siku zinavyokwenda kwa maana wewe ni moja wa maheviweiti humu....dawa ni moja tuu kuwafungia na kutubakiza wachache ili tuongelee mambo ya maana... sasa maadamu na wewe upo pmja nami basi tumia nguvu yako ili tuweze kufanikisha hilo na kuweza kuwafungia watu kama hawa........
 



Kijakazi kumfungia ataanza kulia lia kwamba Lunyungu na kampeni dhidi yangu .Huwa dawa yake ni kumpa ukweli atashikwa na hasira na ataanza matusi then anafungiwa.Yuko kazini anajivua nguo hadi akili na utu wake .Ndiyo madhara haya ya kula pesa za watu na kutumwa kufanya lolote kuwaondoa katika mstari .Mpuuzeni huyu ni mtupu kichwani hadi moyoni .Hana soni na hata tofauti na mafisadi .

Naomba tuendelee kupeana habari kokote na kuhakikisha Vodacome wana elewa kwamba tumechoka kuwa vichwa vya wendawazimu na sasa kuachana nao .Hili ndilo muhimu unaona wana post 2 leo kajiandikisha na anaanza kuparamia hoja .Wandugu JF kusoma ni rahisi kuandika unahitaji akili ya ziada .
 
Hao watu wakikamatwa...Hiyo mali badala ya kuisusia inataifishwa!
Mbona mnazunguka mbuyu?
 
Mushi mada hii haia mahusiano na kumkamata mtu Hawawezi kumkata RA na sisi wanyonge sasa dawa yetu ni kugomea biadhaa za mafisadi .Iwe zao moja kwa moja ama wana mkono ndani yake .This is the only way forward .
 
Mkuu huyu Rostam dawa yake sio kususia huduma ya vodacom dawa yake ni kuuanika ufisadi wake hadharani na njia alizotumia ili mali zake zitaifishwe. Hiyo voda najua ameajiri mitoto mingi ya mafisadi lakini tukumbuke hata walalahoi tupo tunaojipatia kaugali kwa siku.
 

Angalia mahesabu yao kwa siku kwa kukisia tu.

VODA WANA WATEJA 5,000,000. KILA MMOJA AKITUMIA SH.1000.00 TU KWA SIKU WANAPATA SH 5,000,000,000.00. Yaani billion 5 kwa siku moja .Sasa kwa mwezi piga mwenyewe. Linganisha na bajeti ya Tanzania kwa mwaka. Tafakari ..........

Tukigoma ni poa. Nagoma kuanzia leo. NOw I have a reason to quit. Kumbe ni mafisadi again? Walinunua share kwa hela walizoiba EPA, Richie n.k .To hell...BYE VODA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…