Mkwawa alipigana jihad na wajerumani

wazawa

Senior Member
Joined
Jan 29, 2013
Posts
184
Reaction score
58
Kama kungelikuwa n Wakati huu wakati wa vita Kati Ya mkwawa na wajerumani,na Kwa kuwa alikuwa n muislamu je angelionekana pia anapiga jihadi na dunia na watanganyika tungewaona ni magaidi alazwe pema chief Abdul Adam sapi mkwawa muyugumba
 
Kama kungelikuwa n Wakati huu wakati wa vita Kati Ya mkwawa na wajerumani,na Kwa kuwa alikuwa n muislamu je angelionekana pia anapiga jihadi na dunia na watanganyika tungewaona ni magaidi alazwe pema chief Abdul Adam sapi mkwawa muyugumba

Bila shaka isingetafsirika hivyo kwa sababu wakati ule si mkwawa tu pekee aliyekuwa akipigana na hao wavamizi ukisoma historia utaona karibu kila pahala kulikuwepo vita hii
Kwa wakati huu hata leo endapo Wajerumani wakituvamia tutapigana kama nchi yaani Tanzania na wala haitakuwa vita ya Wahehe peke yao na hata kama ingekuwa wanapigana Mkwawa si kweli kwamba chini ya utawala wa Mtemi Mkwawa jamii yake wote ni Waislam kwa hiyo dhana hiyo bado ingekuwa ni batili
 
" Kunyanyua silaha dhidi ya kundi/genge/chama/utawala/Uongozi/elite lolote huo ni ugaidi "

imeshapitishwa rasmi huko USA/UN !!
 
Kwa bahat mbaya nilishindwa kutofautisha uislam wa mkwawa kwa sababu katika makumbusho ya kalenga kuna vijagi kama vitatu kimoja alikuwa anatumia kuangalia upande upi unaangamia kwenye vita baada ya kujaza maji jagi hilo lilikuwa na midomo kama sikosei miwil ambapo upande wake ukibadilika ukiwa mwekundu anakuwa anajua kwamba vita amezidiwa ikitokea upande mwingine anashinda vita, kuna mambo kama kutambika ambayo hayapo kwenye uislam na mkwawa alifanya
 
Mkuu, anayeweza kukubaliana na hilo ni Mzee Mohammed Said na wafuasi wake maana kuna post yake moja anadai Mtemi Kimweri wa Usambaani alikuwa Muislamu na alitumia Shari'a kuwatawala watu wake.

Vv
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…