Spartacus boy
JF-Expert Member
- Sep 22, 2020
- 1,727
- 3,464
Wengi tumekua na kuambiwa na kusoma ya kwamba chifu wa kabila la Wahehe Chifu Mkwawa aka Mkwavinyika Mwamuyinga baada ya kuzidiwa katika vita yake ya mwisho dhidi ya Wajerumank basi alijiua.
Ukweli ni kwamba hakujiua.
Wakati huu wa mwisho vikosi vya Wahehe vilikuwa taabani baada ya jeshi la Wajerumani kuwa na vifaa bora vya kijeshi (wahehe walikuwa na bunduki moja tu ambayo alikuwa nayo mkwawa tu),
Vita ilikuwa bado inaendelea huku Wahehe wakiishiwa nguvu.
Chifu Mkwawa alibakia na 'bodigadi watatu' aliowaamini sana. Mmoja wa hao bodigadi ni mzee Mwanyenza.
(kwa lugha ya kihehe mwanaume kwa jina lake huanza kwa kutamkwa mwa- na kwa mwanamke hurejewa kwa kutamkwa se-) so huyu Mwanyenza ukoo wake ni Nyenza ila jina lake la mwanzo halijulikani.
Baada ya kuona vita imemfikia shingoni mkwawa alitoroka na bodigadi wake hao watatu hadi kwenda kujificha kwenye konde lenye maji na palikuwa na pango.
Akawaambia bodigadi mmoja akatafute digidigi, mwingine akatafute kuni halafu Nyenza abaki naye hapo. Kumbuka muda huo vita bado inaendelea.
Lengo lake ni kwamba hao walioenda kufuata vitu hivyo basi kama ikatokea akivamiwa basi yeye mkwawa na waliobaki wanaenda kusaidia.
Basi wakaondoka. Mkwawa muda huo ndio kabaki na MwaNyenza. Mkwawa akachukua bunduki yake, akamshoot MwaNyenza, akamvisha nguo zake zote yaani kanzu, kilemba (tamaduni ya kuvaa hivi aliifuata kwa waarabu na mkwawa aliupenda Uislam na aliupokea). Kisha baada ya kumuua akapotelea pangoni.
Baada ya bodigadi wale wawili kurejea basi wakajua ya kuwa Mkwawa kauwawa. Wakakimbia.
Wajerumani wakaja na kuuchukua mwili ule wakijua ya Kwamba ndiye Mkwawa mwenyewe.
Wakakata kichwa chake na kwenda nacho Ulaya. Walichotuletea sicho chenyewe
😂😂😂 Yaani walipewa cha Nyenza yaani walipigwa nao wametupiga kutuletea fuvu ambalo silo.
Ndugu wa karibu wa Mkwawa walijua mchezo wote wa Mkwawa so wakawa wanampelekea chakula kupitia watoto wadogo. Chakula kilikuwa kinawekwa kwenye kikapu milulu lakini ndani kuna chombo kingine ninachozuia maji yasiingie na chakula kiwe salama.
Kuna ufundi ulitumika na Mkwawa mwenyewe ambapo hao watoto na ndugu waliokuwa wanaanda chakula walikuwa wanashindwa kutoa siri.
Chakula kilipelekwa kwa siku kadhaa. Kila wakienda walikuwa wanakuta kikapu hakipo maana yake kilikuwa kinapokelewa (na Mkwawa mwenyewe). Ila baada ya siku kadhaa walikuwa wakifika wanaona vikapu vipo palepale na havijaguswa kabisa. Wakapeleka taarifa kuhusu waliyoyaona.
Basi zoezi la kupeleka chakula likaishia hapo na stori kuhusu Mkwawa ikapotelea hapo. Uchifu jina ukabaki kwa mtoto wa kiume wa Mkwawa aitwaye Sapi. Baba yake na spika wa kwanza wa Bunge la Tanzania Adam Mkwawa.
Hii story huwezi kuipata sehemu nyingine kwa sababu tumepumbazwa ila ukikaa na wazee wa zamani basi watakuambia vizuri.
Hata ukienda kwenye makumbusho ya wahehe ya Kalenga utaambiwa tofauti na hii kitu inafichwa.
Hata familia ya Mkwawa hii stori wanaijua fika.
Kwa IQ ya Mkwawa aliyokuwa nayo hakutaka kupotea kizembe.