Mkwaziko: Mama Mkwe kanunua shanga ya mke wangu na yeye mwenyewe mbele yangu

Rufiji dam

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2020
Posts
4,107
Reaction score
9,671
Wadau hamjambo nyoote?

Leo nadhani nimepewa zawadi ya boxing day.

Nilitoka na familia yangu mimi na mke wangu na mama mkwe ambaye kaja tu kusalimia nikaona si ubaya tukatoka tukaelekea Luguluni huko. Tukapata sehemu nzuri tukawa tunaongea maisha.

Mara akapita Mmasai mkononi kashika zile fimbo zao zimejaa bidhaa kibao paap.

Shanga zipo nikazuga kucheza na mtoto huyu Mkwe hana aibu kabisa akamuita wife umeona urembo? Chagua hizo tano kwa pamoja, na mimi nachukua hizi nyembamba, nilipigwa na butwaa hasa haya maisha sijazoea huyu mama hana adabu kabisa.

Nawaza usiku huu niliamshe dude kwa Wife ama nitulie tu. Huyu mama kanivunjia heshima sana. Kuna makabila mengine sio kabisa
 
Hahah *****
Hahah dadeq
 
Nimecheka sana mkuu πŸ˜‚ 🀣 🀣
 
Khsaaa shanga ni mila hizo...
 
Ni kabila gani hao?
 
Mama wakwe wa siku hizi ni vituko. Mama mkwe anaweza kumtamkia binti yake mume wako ni saizi yangu!. Mama wakwe wa siku hizi hawana aibu na soni mbele ya wakwe wana wao, wamekaa kimtegomtego. Ukute uko sawa kiumri au umekaribiana umri au umempita umri mama mkwe hakuna rangi utaacha kuona, huwa wanajiingiza kwenye ligi ya kimapenzi sabamba na binti zao. Hawaoni aibu na soni kuvaa na kuongea isivyo staha, hata kuongea na kutatazama hawapindishi macho pembeni. Huwa tunaona bora mama mkwe awe mzee, hapo kunakuwa na heshima
 
Anajiaibisha tu, wanaume wenyewe hawana hata muda wa kuchezea shanga.

Mwambie mkeo aziweke kwenye beg la mama yake akienda nyumbani kwake akajiulize.
 
Huyo ndo mkwe nayemtaka mm, mkwe hapoi wala haboi anajua kuchangamsha ndoa ya mwanae.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…