Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Kijana wetu wetu alimaliza shahada yake ya uzamili ya ufundi. Alipata ajira za muda mfupi hapa na pale, aliitwa Rwanda, Botswana na kuna wakati alikaa miezi kama mitatu akisaka ajira.
Kuna siku alipata emaile kutoka Afrika ya Kusini. Walimtaka afanye video interview, alifanikiwa hatua ya kwanza na walimuomba a scan vyeti vyake. Kufupisha habari alipata kazi kama fundi mtaalamu huko Kusini.
Baada ya kuzoea maisha alipata binti wa Kizulu wakaanza maisha. Alifunga ndoa na aliita familia yake ishuhudie ndoa yake. Baada ya harusi mama yake alimtembelea sana huko Kusini. Kila mama alipofika hakupenda control aliyokuwa nayo mkwe wetu wa Kizulu kwa kijana wake.
Kumbe mama wa kijana ana ujuzi wa mambo ya Ulimwengu wa kaka Mshana Jr . Usiku mama aliset satellite kuangalia usalama wa nyumba. Kumbe mkwe ana PhD mama alikua mwanafunzi tu. Mkwe alinyuka mama kisawasawa huko angani. Asubuhi wameamka wote damu zimevilia usoni.
Mkwe alimwambia mume wake mama ni lazima aondoke pale kwao haraka na mama akimwambia kijana huyu si mke muache. Mama alirudi Tanzania lakini alipita njia anazojua mpaka ndoa rasmi ilikufa.