Mlela: mwaka huu lazima nioe

Mlela: mwaka huu lazima nioe

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
Msanii wa filamu za Kibongo, Yusuf Mlela amefunguka kwamba baada ya kuishi ‘singo' kwa muda mrefu, sasa anajipanga kuoa hivyo ndani ya mwaka huu lazima ndoto yake hiyo itimie.Msanii-wa filamu za Kibongo, Yusuf Mlela.

Akipiga stori na gazeti hili, Mlela alisema mwaka huu amejiwekea malengo mengi lakini kubwa zaidi ni kuoa kwani anahisi akiendelea kuwa peke yake kuna mambo atakwama kwa kuwa hatakuwa na mtu wa kumshauri kwa karibu.

"Kiukweli maisha yenyewe ni mafupi na umri nao unaenda hivyo lengo langu kubwa kwa mwaka huu ni kuoa na kuhusu nitamuoa nani itajulikana baadaye lakini kwa sasa tambueni kwamba mwaka huu lazima nioe, nimechoka maisha ya ubachela," alisema Mlela ambaye ameingia kwenye Top 3 ya Ijumaa Sexiest Bachelor kwa mwaka 2014-15.
 

Attachments

  • 1422907982801.jpg
    1422907982801.jpg
    56.6 KB · Views: 188
anadhan ndoa ni sawa na kutafuna big jii! ndoa manake uweze kujilea na kumlea utakaye muoa! sasa nae kashazoea kulelewa! atalea wajao?
 
Back
Top Bottom