Ashura9
JF-Expert Member
- Oct 21, 2012
- 740
- 485
Mlenda wa bamia na nyanya chungu
Kuandaa: dakika 10
Mapishi: dakika 20
Walaji: 2
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Mlenda ni mboga yetu cha asili. Kuna mlenda wa aina nyingi sana. Haya mapishi yanaonyesha mojawapo kati ya mlenda unayoweza kuandaa kutumia vitu rahisi – bamia na nyanya chungu, lakini ladha yake si ya kawaida. Inafaa zaidi kuliwa na ugali ukiwa wa moto na pilipili.
Mahitaji
Maelekezo
Kuandaa: dakika 10
Mapishi: dakika 20
Walaji: 2
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Mlenda ni mboga yetu cha asili. Kuna mlenda wa aina nyingi sana. Haya mapishi yanaonyesha mojawapo kati ya mlenda unayoweza kuandaa kutumia vitu rahisi – bamia na nyanya chungu, lakini ladha yake si ya kawaida. Inafaa zaidi kuliwa na ugali ukiwa wa moto na pilipili.
Mahitaji
- Nyanya chungu
- Bamia
- Nyanya maji
- Kitunguu
- Karoti
- Pilipili hoho
- Mafuta ya kupikia
Maelekezo
- Menya nyanya, kitunguu, karoti na pilipili hoho. Kata kwenye vipande vidogo.
- Andaa bamia kwa kutoa ncha na mkia kisha kata mara mbili au jinsi utakavyopendezwa
- Menya nyanya chungu na kuikata katikati.
- Bandika sufuria kisha weka mafuta kiasi. Yakichemka weka nyanya chungu. Kaanga kama dakika kumi ili zibadilike rangi na kuwa za rangi ya udongo (angalia zisiungue). Kisha zitoe kwenye mafuta.
- Punguza mafuta ya kula kiasi, bakiza yanayotosha kupikia mboga.
- Weka kitunguu. Koroga na subiria kiive.
- Weka pilipili hoho na carrot. Koroga kwa muda wa takribani dakika 3
- Weka nyanya. Koroga na kisha funika ili ziive.
- Weka bamia. Ongeza maji kiasi. Bamia huchukua muda kuiva, hivyo ni vizuri kuongeza maji.
- Funika mboga yako na acha ichemke kwa muda wa dakika kama 10 – 15. Bamia zitakua zimeiva. Kuwa makini bamia zisilainike sana.
- Weka nyanya chungu kwenye mchuzi. Acha zichemke kama dakika 5 kisha ipua mboga yako inakua tayari kuliwa.
- Jirambe na ladha ya maisha, maisha ya kuteleza kama ulivyo mlenda