Mlevi, mzee wa kupiga hesabu baada ya matumizi

Nasikia ukilewa ndio unaonesha tabia yako halisi 😂😂
 
Kumbe walevi tuna tabia za kufanana eeh! Hata mimi huwa natoa nyekundu tu zile chenji nazilundika tu mfuko wake. Kunavyokucha unakuta kibunda chote kimekuwa chembamba unaogopa hata kuhesabu. Shikamoo pombe.
 

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kumbe walevi tuna tabia za kufanana eeh! Hata mimi huwa natoa nyekundu tu zile chenji nazilundika tu mfuko wake. Kunavyokucha unakuta kibunda chote kimekuwa chembamba unaogopa hata kuhesabu. Shikamoo pombe.
Swali, hivi kwanini huwa tunaogopa kuhesabu wakati tutahesabu tu?
 
Yaaan sisi walevi tuna mateso na raha zinazo fanana. Mahesabu ya asubuh hua yanaumiza sana roho. Ukipanga kutoka na pesa kidogo gambe likinoga unavuta pesa kwa cm. Ukipanga kutoka pekeako ili usitumie pesa nyingi unakutana na washikaj from nowhere au unawaita mwenyew. Ukiwa na hela hutak kutoka home usiku usingiz hauji unajikuta unajiambia ngoja nikanywe bia 3 nirudi kulala unajikuta umekesha hukohuko...
All in all pombe zina chuma ulete maana zile hesabu za asubuh hazijawahi ku balance 😂
 
Leo nimeamua nijilipue maana nimevurugwa sana...
Pombe hizi!! [emoji36]
 
Mleta mada umeandika ukweli mtupu,hii inatutokea wengi sana mpaka saingine nahisi sjui nimelogwa!!! Unakuta umetoka na bajeti ya maybe laki pombe zikikolea unaenda Atm kuchomoa mpunga ..asubh ndo kukikucha pombe zimeisha kichwani unaanza waza hela umetumiaje!? Jinsi ulivoandika ni kama unanisema mm yani.
 
Mm nikajuaga ni mm mwenyew inanitokea kumbe tuko wengi tunapitia maswahibu haya.
 
Hahahaha hii ya kuita washkaji Kama unanisema mimi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…