SoC02 Mlezi siyo pesa

Stories of Change - 2022 Competition

babu kavu

Senior Member
Joined
Jul 4, 2022
Posts
120
Reaction score
128
NI wazi kuwa Kasi ya maisha imekuwa Kali kiasi kwamba si baba Wala mama ambaye anataka kukaa nyumbani na kusubiri bili za mwisho wa mwezi kuanzia , umeme, maji,usafi,ulinzi,school bus fees n.k
Bado hatujagusia gharama za chakula, maradhi, mavazi na Ada za shule kwa waliobarikiwa kuwa na watoto,kichwa lazima kiume na lazima tusaidiane.

Mke na mume watakapotoka kwenda kutafuta watahitaji dada wa kukaa na kuangalia mazingira ya nyumba na watoto kwa ujumla,wanaagizia binti mdogo kutoka mbali ambaye atakubali kulipwa kiasi Kidogo Cha pesa na wanakuwa hawana Mambo mengi hivyo hawatasumbua sana,lakini Kuna suala kubwa na la msingi huwa wanajisahau kujiuliza.

  • Huyu msichana anatokea katika maadili gani!?
  • Ana tabia zinazoruhusu kubaki na watoto zetu na kuwa na uhakika kuwa watoto atawaangalia kama wewe mzazi unavyotaka!?
  • Mila na desturi za kwao ni nzuri kwa malezi ya mwanao!?
hakika maswali ni mengi ,ila kwa sababu tunahitaji kutoka kwenda kutafuta Basi tunapuuzia haya maswali

Tusimtafute mchawi nani kwenye mmomonyoko wa maadili kwa kizazi hiki.Baba umejisahau sana zamani baba anaoa kwa kuangalia mama mwenye maadili kwa ajili ya kuja kulea watoto wake lakini Sasa hivi tunaangalia uzuri na anafanya kazi gani,madhara yake tunapata watoto "pisi" Kali na sio watoto "wazuri" ,ambao wanalelewa na binti aliyetoka kijijini ambao ni "washamba" televisheni kuwasha anafundishwa na mtoto anayekuja kumlea,simu anayokabidhiwa kutumia anafundishwa na mtoto anaye muangalia na mbaya zaidi ni mtoto kumlea mtoto(maake ncheke kwanza)

Kuna rafiki yangu aliniambia anataka kuoa lakini anataka msichana anayefanya kazi ili wasaidiane kutafuta pesa,ni muda sasa umefika vijana wa kiume tubadili maana ya kusaidiana kwamba baba akahangaike asubuhi mpaka usiku lakini mama akahangaike asubuhi mpaka mchana akaangalie watoto wake na kujua maendeleo ya ukuaji kiakili na kitabia kwa mtoto I'll kupata kurudisha kizazi kilichokuwa kinapisha mtu mzima kwenye siti akae na yeye kusimama.

WANAUME TUONGEZE KASI YA KUTAFUTA ILI MAMA APATE MUDA WA KUIANGALIA FAMILIA
 
Upvote 1
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…