Ilivyo, kila dini ina vyuo vyake wanakofundishana imani zao huko, kuna madrasa za waislam wanafundishana tangu watoto wadogo huko wanakokutana, kuna bible study wakristo wanafundishana huko makanisani na vyuo vyao kulingana na imani za madhehebu yao na imekuwa hivyo bila mikanganyiko. Ukitaka uchungaji unaenda chuo chake cha dhehebu unalotaka kwa mujibu wa imani uliyonayo. Hao wa maseminari nao wana utaratibu wao wa kupata elimu ya dini na imani zao. Inakuaje sasa mambo hayo ya dini yaingizwe kwenye mitihani ya taifa? Ndio, ilikuwepo islamic knowedge na bible knowldge kama masomo yasiyokuwa na msukumo mkubwa hata ukipata A haihesabiki katika kuomba ajira au kozi ya kitaalam. Eti sasa hayo masomo ya pembeni yameingizwa rasmi na kuundiwa comb. Kwa hiyo nikitaka kuwa sheikh/mchungaji maksi zangu zita be regarded na NECTA. Sasa hapa serikali ndio imejiingiza kwenye dini au dini ndio imejiingiza kwenye serikali? Huu ni mkanganyiko mtupu katika taifa lisiloongozwa kwa misingi ya dini