mama dunia
JF-Expert Member
- Dec 22, 2011
- 420
- 84
Yaani nilifikiri wizi umedhibitiwa pale mlimani city kumbe bado bwana, yaani jana majira ya saa saba mchana nipo zanguu pale karibu kabisa na nilipopack kuna vijamaa viwili si vilikuwa vinaiba/yaani vishatoa site mirrors sijui nafikiri ndo walikuwa ktk process za kutoa na power window, sasa mmoja wao si akachoropoka gafla akabakia mmoja, amepewaje kipondo, yaani domo lilivimba, damu nk...tena jamaa mwenyewe ukiambiwa ni mjikibaka huwezi amini, jamaa mashallah handsome, kajazia jazia kidogo, mtanashati etc, yaani Dar ni zaidi ya ujuavyo , unaweza fikiri jamaa ana kazi zake kumbe mwizi, so kuweni makini pale. Jamaa wa gari iliyokuwa inakwapuliwa vitu alimind kichizi yaani X-trail mpyaaa ikawa ndo hivyo tena......