Mlinzi wa kura wa chama tayari yupo ndani kwenye kituo huo wizi utafanyika saa ngapi?
Hivi kwa akili zako kama lengo ni kuiba kura NEC inayo simamia uchaguzi nchi nzima, yenye idadi ya watu kamili waliojiandikisha, wao ndio wa kwanza kupata data ya watu waliojitokeza na shortfalls za uchaguzi; kama ni kuchakachua kwanini waangaike na sehemu ambazo kuna watu wengi wakati wana system wanayo manage wao, wanasimamia uchaguzi sehemu zingine hata wagombea wa majimbo hawawezi kwenda piga kambi let alone viongozi wa UKAWA.
Kama kulinda unalinda vipi zaidi ya kuwa na msimamizi ndani na kujua procedures zikoje, kukaa nje ya vituo unahesabu vipi kura wakati hesabu zinapigiwa ndani ya ukumbi.
Safari hii kwakweli watu somo wasipolipata sisi raia wapenda amani tunapenda kuona polisi wakiwashikisha adabu hawa vijana wasiotaka kutii amri za sheria kwa malengo ya kuleta fujo ambazo viongozi wao wana hubiri kutwa kwanza democratic indicators zote tayari zishaonyesha Magufuli for president na UKAWA wamejichimbia kaburi wao wenyewe.
Linapokuja suali la
kulinda kura ni kwamba wahusika tayari wamekosa imani na
system nzimainayohusika na kusimamia uchaguzi huu yaani
NEC na Polisi. Hapo nitakufafanulia pengine itakusaidia kuujua ukweli!
NEC na watendaji wake si huru na hata wewe unalijua hilo!
Tume yote ya uchaguzi pamoja na wasimamizi wote wa uchaguzi wanachaguliwa na Mwenyekiti wenu wa CCM. Huu ni uchaguzi wa vyama vingi Tanzania na sio uchaguzi ya wagombea wa CCM tu! Labda nikukumbushe tu kwa mfano mara tu baada ya kumalizika kwa zoezi la kurejesha fomu za kuomba kugombea ubunge kwa tume ya uchaguzi basi wasimamizi wa uchaguzi
zaidi ya tisa waliwapa ushindi wagombea ubunge waCCM ushindi wa bila ya kupingwa! Yaani walitaka kupiga bao la mkono mchana kweupe! Kama ingekuwa uchaguzi ni mchezo wa mpira wa miguu basi ni kwamba
Refa na washika vibendera wote ni wa upande mmoja!
Hao
Polisi ndio hata kipofu anaona ya kwamba wao ni CCM zealots(wanamaskani)! Polisi ni kama
wamehasiwa kuwachukulia hatua wanaCCM wanapovuruga amani.
IGP na makamishana wote wa polisi wanachaguliwa na Mwenyekiti wenu wa CCM. Sawa ndio katiba inavyosema lakini
sheria ni msumeno jamani. Hivi katika uchaguzi huu basi wanaofanya fujo ni wanachama na wagombea wa upinzani tu? Ebu nikukumbushe tena katika uchaguzi wenu wa maoni tu basi tumewashudia kuanzia wagombea ngazi zote - urais, ubunge na udiwani-
wakipigana ngumi hadharani pamoja na kugawa rushwa nje nje! Kuna ushahidi na uthibitisho wa picha na video za kina Ndugai, Kamala na yule aliotaka kugombea urais kupitia chama chenu wakipigana ama kupigwa hadharani. Hatukusikia Polisi kuchukua hatua yoyote. Hio rushwa kwenye CCM ndio hata sitaki kuitaizungumzia maana inajulika wazi ya kwamba
CCM ni chama cha Rushwa .Wagombea ubunge wa upinzani Msigwa, Masha, Ester Bulaya, Lema na wengine wengi tu tayari wamepelekwa mahabusu. Hapo naona kabakia huyo Lowasa tu kupelekwa mahabusu!
Hapo nimekupa picha tu ya kwamba System nzima inayohusika na uchaguzi huu imeegemea upande wenu wa CCM. Ingelikuwa ni pambano la mpira baina ya
Simba na Yanga basi ni sawa na mfano huu: Pambano linachezwa Jangwani, Refa ni mwenyekiti wa klabu ya Yanga, washika vibendera ni makamo mwenyekiti wa Klabu ya Yanga na katibu mkuu wake. Hata wale ball boys hapo jangwani basi ni Polisi. Simba imebakiwa na watazamaji tu! Sasa jee unatarajia matokeo gani hapo. Kwa picha hio ni kwamba
UKAWA ni lazima walinde kura zao lasivyo watapigwa mabao!