Mlinzi wa Manchester City, Benjamin Mendy (27) ameshitakiwa kwa makosa manne ya ubakaji na lingine la unyanyasaji wa kijinsia

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Mlinzi wa Manchester City, Benjamin Mendy (27) ameshitakiwa kwa makosa manne ya ubakaji na lingine la unyanyasaji wa kijinsia, kwa mujibu wa Polisi wa Cheshire.

Makosa hayo yanawahusu walalamikaji watatu walio na umri wa zaidi ya miaka 16 na yanaelezwa kufanyika kati ya Oktoba 2020 na Agosti mwaka huu.

Mendy, anayeishi eneo la Prestbury, kwa sasa anashikiliwa na polisi kabla ya leo kufikishwa mahakamani katika mahakama ya mkoa ya Chester.

Mlinzi huyo wa kushoto amekuwa akiwachezea mabingwa hao wa ligi kuu England msimu uliopita tangu mwaka 2017 alipojiunga nao akitokea Monaco kwa ada inayoripotiwa kuwa ni £52m.

Msemaji wa Polisi alisema: "Polisi Cheshire na kitengo cha mashataka cha Crown wanapenda kuwakumbusha kuwa kesi ya jinai inayomkabili Mendy ipo na ana haki zote za kusikilizwa."

Manchester City ilisema mlinzi huyo, ambaye pia anachezea timu ya taifa ya Ufaransa , ameondolewa kwenye kikosi hicho mpaka baada ya uchunguzi wa kesi yake hiyo.

"Suala hilo liko kwenye mchakato ya kisheria kwa hivyo klabu haitaweza kuzungumzia zaidi mpaka litakapokamilika," Klabu hiyo iliongoeza.


BBC
 
Pesa mbaya inakufanya ujione uko juu ya vyote, kumbe sheria zipo, amesimamishwa na klabu yake mpaka balaa lake liishe.
 
UK wana sheria kali za kulinda haki za wanawake. Wachezaji wahuni wahuni hukurupuka kule
 
Hizo ni kesi za kubambikiza ambazo ma-star wengi wa marekani hukumbana nazo. Lengo hapo ni pesa tu.
 
Pesa mbaya inakufanya ujione uko juu ya vyote, kumbe sheria zipo, amesimamishwa na klabu yake mpaka balaa lake liishe.
Dunia ina siri nyingi sana mkuu, sometimes ukionaga hao mastaa wameshtakiwa is not always kwamba wamekosea or kama wamekosea jiulize why makosa wanayo shtakiwa nayo mbona ya miaka kadhaa iliopita? Hao waliokosewa leo ndio wamegundua kama walikosewa? Narudia, DUNIA ina SIRI nyingi sana tusizo zijua!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…