Mlio kwenye ndoa kuweni makini, ona huyu alichofanywa

Mlio kwenye ndoa kuweni makini, ona huyu alichofanywa

Mahunguchila

Member
Joined
Jun 11, 2012
Posts
74
Reaction score
34
Habari zenu wana jamii,

Leo nina ushauri kwa wale walioko kwenye ndoa, na nimeona niwape ushauri huu kufuatia yalompata dada yangu.

Dada yangu aliolewa miaka ya 1990 na baba mmoja ambae by that time alikuwa mfanyakazi ktk shirika moja la uma. Alifukuzwa kazi, na sifahamu sababu ya yeye kufukuzwa kazi miaka ya 2000. Toka hapo sister kwa upendo aliishi na shemeji na hakuwahi kumsimanga kwa kutokuwa na kazi na mahitaji yake yote yalitimizwa na sister.

Sister alikuwa mfanyakazi wa benk na kwa kweli kifedha alijiweza. Alimwamini sana mumewe na maisha yao yalikuwa ya upendo na amani. they had 4 kids. Wakati dada akimwamini sana mumuwe, kumbe mumewe alikuwa akifahamika mtaani kwa jina la POPOBAWA! Alikuwa MALAYA wa kupindukia! All those days ni kama sister alikuwa kafungwa akili kwani hata siku moja hakuwahi dhani kuwa the famous popobawa pale mtaani alikuwa ni mumewe. Alikuja kupoteza imani na mumuwe baada ya kumkuta usiku akufanya ngono na house girl wao jikoni.

Hofu ya kupata maambukizi ya Ukimwi ilitawala maisha yake, na hakuchukua muda aliugua na kufariki kwa VVU.

USHAURI: Kuna slogan moja ya wanajeshi, inasema TRUST NOTHING SUSPECT EVERYTHING! Pamoja na kuwa mnaaminiana sana na waume/wake zenu lakini jaribuni kuwa makini sana katika huu uaminifu kwani wanandoa wengi wamekuwa wakitumia neno kuaminiana vibaya! Mume hataki mke aguse simu yake, na ikitokea hivyo basi atalalamika mke wangu huniamini na wakati huo huo ana vimada zaidi ya kumi na anataka aaminike kwa mkewe.

Ni mtazamo wangu tu Mahunguchila.
 
Miaka zaidi ya 12 imepita...ok RIP ur sister
 
Asante kwa somo zuri........ lakini ndio ukweli unaoumiza rate ya VVU iko juu zaidi hasa kwa wanandoa
 
mnh usitoke,ukitoka basi tumia condom....:whistle:
 
hii ni balaa tupu acha tu... RIP your beloved sister..
 
Yaani huwa inakera mtu anapokuwa mwaminifu alafu mwenzie ndo ivyo tena cha wote.
Yaani suala la uaminifu kwenye ndoa ni gumu bse lina involve watu wawili wenye background tofauti.
No wonder nowdays maana ya ndoa inapotea with time.
Mtu yuko ndoani anagawa kama hana akili the same na kwa wanaume anapiga nje utadhani ameaidiwa bonus!
 
Tupo wangapi,julishaneni 1,2,3 na 4..kuna bint akipita hapa atatema cheche !
 
mpe pole maana maisha kweli ni majuto hakutegemea ila Mungu atamuepusha na huyo popobawa
 
so sad........

Jamani wanandoa mlinde afya na uhai wa wenza wenu..... Wengine wanadai mwanaume hawezi kuwa na mwanamke mmoja, qanadhani sifa kuwapanga mstari.....

Wenye mafiga matano pia muache
 
dah, ukisikia ukweli mchungu ndiyo huu.... yaani dada alikuwa yuko so committed kwenye ndoa yake, at the end of the day analetewa virusi humo humo ndani..
 
Mtandao wa ngono ni mkubwa kuliko tunavyodhani na normally unapostukia game wewe unakuwa wa mwisho maana wengineo wote wanaokuzunguka wanakuwa tayari wameshanyaka issue.....
 
Mi ndo maana nilishasema upelelezi ni muhimu. Mi napekua kuanzia begi mpaka simu. Nyie mnaokalia ooh utakufa kwa pressure; si kila mtu ana chance ya kuugua pressure (me included) ila kila aliye na wapenzi wengi au kwenye mtandao wa wapenzi wengi ana chance kuubwa tu ya kufa kwa ngoma. Napekua ili nijuage mapema kama naishi na popo bawa nichape lapa kabla ya kufa na kuacha wanagu niwapendao kuliko chochote kwenye hii dunia.
 
Habari zenu wana jamii,

Leo nina ushauri kwa wale walioko kwenye ndoa, na nimeona niwape ushauri huu kufuatia yalompata dada yangu.

Dada yangu aliolewa miaka ya 1990 na baba mmoja ambae by that time alikuwa mfanyakazi ktk shirika moja la uma. Alifukuzwa kazi, na sifahamu sababu ya yeye kufukuzwa kazi miaka ya 2000. Toka hapo sister kwa upendo aliishi na shemeji na hakuwahi kumsimanga kwa kutokuwa na kazi na mahitaji yake yote yalitimizwa na sister.

Duh, hii kali!
 
Yaani huwa inakera mtu anapokuwa mwaminifu alafu mwenzie ndo ivyo tena cha wote.
Yaani suala la uaminifu kwenye ndoa ni gumu bse lina involve watu wawili wenye background tofauti.
No wonder nowdays maana ya ndoa inapotea with time.
Mtu yuko ndoani anagawa kama hana akili the same na kwa wanaume anapiga nje utadhani ameaidiwa bonus!

Ameahidiwa bonus, ha ha ha ha...
 
Back
Top Bottom