Ziroseventytwo
JF-Expert Member
- Mar 27, 2011
- 8,581
- 15,618
Katikati ya miaka 2000, ilikuwa 2006 Tuliingia ubia mimi na jamaa yangu tukanunua gari aina ya Mitsubishi Fuso fighter 17. Gari tuliiagiza kwa kumtuma mtu tuliyemwamini. Kwa wakati ule tulimpa Us$ 9700, alituambia kuwa hizo zilitosha kwa kila kitu.kuanzia kununua, kusafirisha, ukaguzi nk. Baada ya miezi kama m4 gari ikafika. Tukaanza kazi ya kuitoa pale bandarini. Tukalipa kodi, ushuru na tozo nyingine kibao pale bandarini hatimae tukalitoa.
Baada ya wiki tukafanya mpango tukaenda kuweka body pale Tabata dumple. Kazi ikaisha na baada ya process zote gari ikasimama ikiwa na thamani ya 24ml. Tukaenda bima tukakata comprehensive 12% ya thamani ya gari ambayo tuliishusha mpaka 15m na kulipa kama 1.8ml.
Tukaanza kazi. Tukapambana kufa kupona, usiku mchana. Kumbuka tulitoa kila m1 13ml. Sikuwahi kuishika ile 13ml mpaka tulipoamua kuja kuuza gari miaka mi4 baadae. Tukauza ile gari kwa 16ml baada ya kuanza kusumbua.
Nachotaka kusema hapa ni nini.
Wakati sisi tunanunua gari thamani yake ilikuwa 24m. Kwa sasa ukilitaka na ukapitia process nilizotaja hapo huu ni 50-55ml
Wakati ule tyres zilikuwa wastani wa Tsh 150-170k kwa sasa ni 370-400k
Mafuta diesel lita ilikuwa 850 wakati sasa ni 2000. Rim ilikuwa 25k kwa sasa ni 150k. Mzigo wa spring ulikuwa ni kati ya 50k-60 kwa sasa huwezi pata chini ya 250k
Ukiangali gharamaza uendeshaji wa gari zimepanda zaidi ya mara 2. Kwa uzoefu wangu gharama za kusafirisha mzigo toka eneo moja kwenda lingine pesa iliyoongezeka ni kama elfu 2000. Sisi tulikuwa tukitokea labda kibaigwa tulikuwa tunatoza wastani wa shs 500000 kwa tani 10. Kwa sasa ni wastani wa shs 700000 kwa tani 10.
Ushauri.
Kama unataka biashara ya gari aina ya fuso iwe tandam. Hiyo inabeba wastani wa tani16 kwa ingine ile ile ya single. Mafuta ya kutoka dom mpaka dsm tofauti ni lts10. Traffic ukiwapa 5000 hata yule wa single naye anatoa 5000 pia. Kila unachofanya kwa single ndio unachofanya kwa tandam. Tofauti ni zile tyres 4 zinazoongezeka. Uzoefu unaonyesha mwenye single ndio anaongoza kwa kumaliza tairi kuliko wa tandam.