MINOCYCLINE
JF-Expert Member
- Apr 2, 2015
- 8,018
- 16,802
1. Kujiona ( Kujimwambafai ) kabla ya Mchezo kuanza kwa Mshambuliaji Hatari wa Yanga SC Fiston Mayele kulichangia Kumharibu / Kumharibia Kisaikolojia kwani Kitendo kile ni kama vile kiliwapa Kengele Mabeki wa Simba SC waongeze juhudi maradufu katika Kumdhibiti hadi akashindwa Kufurukuta.
2. Upumbavu, Utoto, Ushamba na Nidhamu mbovu ya Winga Mshambuliaji wa Simba SC Bernard Morrison kulichangia kwa 85% kumtoa katika Mchezo na hata Kuikosesha Simba SC Ushindi kwani endapo angekuwa na Maadili ya Kimchezo na kuamua kweli Kucheza Mpira jana angekuwa ni Tishio zaidi na hata Kuwafunga Yanga SC ingewezekana.
3. Kwa mara ya Kwanza Pongezi ziende kwa TFF na Bodi ya Ligi kwa Kumchagua Mwamuzi ( Refa ) Kayoko na Wasaidizi wake Wote kwani walichezesha vyema, kwa Ustadi na Uweledi mkubwa na hakika Wanastahili hata Tuzo kwa Kazi iliyotukuka.
4. Beki wa pembeni Kibwana Shomary ameonyesha kuwa ni Hazina si tu kwa Yanga SC yake bali hata kwa Taifa ( Tanzania ) kwa Uwezo mkubwa alionao ambao hauendani kabisa na Umri wake Mdogo.
5. Beki wa Simba SC Henock Inonga Baka ametoa Darasa tosha kwa Mabeki wote wa Tanzania na wale ambao wana Kazi ya Kumzuia Mshambuliaji Hatari wa Yanga SC Fiston Mayele kuwa watumie sana Akili na siyo Nguvu halafu Wajiamini muda wote.
6. Makocha wa Yanga SC na Simba SC wametnibitisha kuwa uwepo Wao kama Makocha katika hivi Vilabu Vikubwa nchini si wa Makosa au wa bahati mbaya. Pongezi Kwao Wote.
7. Jana Watanzania, Afrika na hata dunia imeshuhudia Derby ya Kibabe kweli na Wametufurahisha Watazamaji wote.
Aksanteni sana Yanga SC na Simba SC.