Mliofanikiwa, Mlitumia Mbinu Gani kwa mfumo Huu Wa Maisha kama Wangu?

Majigo

JF-Expert Member
Joined
Feb 23, 2012
Posts
5,519
Reaction score
1,828
Salam za Upendo kwenu nyote .........Kutokana masaa 8 ninayotumia Nikiwa Chuo ...... Sasa Naona Mambo Yanakwenda Sivyo ...... Hasa Ktk kabiashara kangu kanakonifanya Nipate Pesa Za Kujikimu na Kuendesha Shughur Zangu za Masomo (ngazi ya Cheti) .... Nilzan nitaweza kusoma Na Kufanya 2biashara 2dogo2dogo.... lkn mda mwingne najikuta hata Hela Ya Kula Nakosa kabisa......Jaman nitumie Mbinu Gani Ili Niweze Kufanikiwa Kwa Mfumo Wangu huu Wa Maisha Ya biashara Na Masoma bila athari zozote?....Ushaur/pendekezo/maoni Toka Kwenu Ni Muhimu Sana..... nami Nitakubali kujipanga Upya!
 
Pole, pambana tu mjeshi. Watakuja kukusaidia. Mimi nilimaliza kusoma kila kitu ndo nikaingia mzigoni. pole na usikate tamaa yawezekan. Wapo waliofanya ivyo y nat ya?!
 
Pole, pambana tu mjeshi. Watakuja kukusaidia. Mimi nilimaliza kusoma kila kitu ndo nikaingia mzigoni. pole na usikate tamaa yawezekan. Wapo waliofanya ivyo y nat ya?!
ahsante Kwa Kunipa Moyo Ndugu Yangu...Mungu Akulipe Heri, Kwa Mda Wako Ulioutumia!
 
Mkuu Mafanikio ni Mchako ni kama ilivyo michakato ya Chama Kuja kushika Dola, so mara nyigi vitu kama kusua sua huwa vipo sana na hata biashara kufa kabisa ila zote i hatua muhimu sana atika Maish ya Ujasirimali na kinacho takiwa ni kuendeea kupambana n kujlibu kucheki tatizo liko wapi na kutatua hilo tatizo, Biashara hiwezi kufa bila kuwa na tatizo, so ni vizuri ukacheki sababu kuu inayo pelekea kuwa hivyo
 
Uko Sahh Kabisa Kiongoz Wangu CHASHA Nami Nimegundua Kuwa Pamoja Na Yote Lakn Mda Ndio Tatizo Kubwa Sana,....... Niko Hapa Ili Kupata Mawazo Kwenu Na Hasa Wale Waliofanikiwa kujisimamia Kimasomo Na Huku Wakiwa Na Jambo Jingne Hasa Biashara.....Wali/Wanatumia Mbinu Gani Ambayo haikuwasumbua Ktk Kufikia Lengo
 


Muda sio tatizo,......ni wewe tu kwenye kuweka vipaumbele vyako. Anza na kupungunguza muda unaotumia online.....JF, FB etc!

Give energy to things that give (or will give) you energy.
 

Hii ndio faida mojawapo ya kuanza biashara katika katika kiwango chako, kwan inakuwia rahisi kutambua changamoto mapema na kutafuta namna ya kukabiliana nazo. Ujuzi utakaoupata katika kukabiliana na changamoto hizo utakusaidia sana pale kampuni au biashara yako itakapokuwa. Ujuzi huo pia unaweza kutumika katika kuikuza biashara yako. Kitu pekee kikubwa na muhimu tunachoweza kukuambia kwa sasa, ni vyema ukaanza kufikiria suala la kuwa na msaidizi. Si kutafuta tu mtu na kumuachia biashara bali unatakiwa umgroom mtu wako utakayemuona ni sahihi (Mentoring). Katika mchakato huo ukigundua kuwa culture ya mtu unayemgroom inaendana na ya biashara yako, basi shukuru Mungu kwani umepata mtu sahihi.

Sasa ninaomba nitumie mfano mmoja wa mwanachama wetu (nitamuita John) kwani naye alipitia safari kama hii unayoipitia wewe sasa hivi. John alianza biashara kama mfugaji wakati anasoma shule ya msingi, alipochaguliwa kujiunga na elimu ya sekondari aliikabidhi biashara kwa familia yake ili wamsaidie kuitunza. Hata hivyo kipindi cha likizo John alikuwa anakumbana na hali ya kukatisha tamaa na kusikitisha kwani alikuwa anagundua mapungufu makubwa katika mifugo yake. John alipomaliza kidato cha nne aliamua kuuza mifugo yote, na hivyo kujipatia kiasi kikubwa cha fedha kama mtaji wa kuanzisha biashara nyingine. Alipofika huko alitafuta mtu wa kushirikiana naye kwenye biashara (George) kwani alitambua kuwa ili biashara ikue basi hana budi kutafuta msaidizi. Biashara ilianza na kuendelea vizuri

Baada ya miezi saba John alitakiwa akajiunge na High School kwan matokeo yake yalikuwa ni mazuri sana. Ilimlazimu John kuiacha biashara katika mikono ya msaidizi wake. Hata hivyo katika kipindi cha miezi sita tu baada ya John kuondoka biashara ilikufa, tena kwa uzembe na ufujaji wa George. John aliingiwa na roho ya kukata tamaa hasa ya kufanya biashara kwani jasho lake lote tangu shule ya msingi lilipotea hivi hivi, baada ya kumaliza kidato cha sita John hakuwa tena na mtaji wa kufanya biashara hivyo aliamua kuajiriwa, hata hivyo baada ya kipindi cha mwaka mmoja John aliachana na ajira hiyo na kujiunga na elimu ya Chuo kikuu. Katika kipindi cha mwaka mmoja alichokuwa kazini John aliweza kujiwekea akiba ya kutosha kuanza biashara, lakini changamoto ilikuwa atamudu vipi kufanya Biashara na Masomo kwa wakati mmoja? Mawazo ya kuanzisha biashara na kumkabidhi mtu yalikuwa yanamjia mara kwa mara, lakini kila akikumbuka kilichotokea nyuma aliamua kuyapuuza.

Hata hivyo John alifikia hitimisho kwamba ataanza biashara na kuisimamia mwenyewe, na biashara hiyo ataanza katika chumba chake cha kulala huko huko chuoni. Kukidhi makitaji ya Biashara hiyo ilimbidi anunue, Computer, Printer, Binding Machine, Scanner na Paper Cutter. Biashara ikaanza na wanafunzi wakawa wanapata huduma baada ya vipindi. Hata hivyo demand ya huduma zake ilivyoanza kukua kwa kasi changamoto mpya zikajitokeza; kukidhi mahitaji yote ya wanafunzi na kwa wakati, pamoja na suala la usimamizi. John alikaa chini na kutafakari matatizo yaliyochangia kuiangusha biashara yake ya awali, akiamini kuwa kutambua matatizo hayo kutampatia elimu tosha juu ya nini cha kufanya katika biashara hii mpya...
Itaendelea

 
siri kubwa ni kujituma na kusimamia malengo yako,utapambana na changamoto,lakini hutakiwi kukata tamaa,simamia unachokiamini na fanyia kazi kile ulichokipanga,kuwa mvumilivu.
 
Kwakweli hili ni somo nzuri sana hasa kwa sisi ambao tunataka kuanzisha biashara lakini tunaogopa kuanzisha. Hii inatokana na ukweli kwamba aidha hatujui namna ya kuiendesha au hatuna uzoefu wowote wa kuendesha biashara.Hili kwetu ni somo tosha
 
Tunaomba masomo haya ya uelimishaji yaendele ili nasi tuweze kujifunza na tuwe wajasilimia mali wazuri na hatimaye wafanyabiashara wakubwa
 
biashara nyingi zinakufa kwa sababu ya mitaji midogo na usimamizi mbovu tumeona ishu ya John ameanza kidogo lakini wateja wamekuwa wengi hivyo inabidi aongeze mtaji ili kutopoteza wateja na aweke mfanyakazi kwa vile John yuko chuoni itakuwa rahisi kumsimamia na mwenye uzi kama biashara yako iko mbali na chuoni kwako na umeweka mtu hapo uaminifu ni mdogo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…