Mliokosa mikopo HESLB uanganeni!

Tulimumu

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2013
Posts
14,409
Reaction score
13,262
Mwaka 2002 serikali ilwanyima mikopo wanafunzi 603 waliochaguliwa UDSM. Wale wanafunzi waliripoti chuoni na kuungana kudai haki ya kukopeshwa. Baada ya shinikizo kubwa wanafunzi wote walikopeshwa/dhaminiwa na serikali. Asiwadanganye mtu. Si kweli kuwa serikali haina pesa bali haijui vipaumbele. Kama inaweza kuawapeleka maelfu jeshini na kuwahudumia kwa kila kitu bila mkopo itakuwaje leo iseme haina pesa? Kama inaweza kutenga mamilioni kwa ajili ya kukimbiza na kuzima mwenge, itakuwaje isiwe na pesa za kukopesha wanafunzi? Ni lini mlisikia rais ameahirisha ziara zake za kuizunguka dunia kwasababu serikali haina pesa? Ni lini mlisikia wabunge wamekosa posho zao kwakuwa serikali haina pesa?Mmeambiwa waziri mkuu analipwa milioni 26 na rais milioni 32 kila mwezi. Ni lini mlisikia serikali imeshindwa kuwalipa? Ukweli ni kuwa serikali ina pesa za kukopesha wanafunzi wote waliodahiliwa lakini inaelekeza pesa kwenye mambo yasiyo na msingi. Uanganeni mdai haki zenu kwani hizo ni pesa wanazokamuliwa masikini wa nchi hii. Kama pesa hakuna, waliwapeleka jeshini kufanya nini? Muda mliokaa jeshini si mngekuwa mmewasaidia wazazi kutafuta pesa za kujigharimia? Sasa hivi wamewaita wengine tena jeshini, hizo pesa zintoka wapi?! SOLIDARITY FOR EVER?
 
yan bro kiukweli inauma sana sana yan inauma sana jaman roho inauma kiukwel
 
Hili sio kwa waliokosa2, hii ni vita ya wote, uliyepata, wazazi, wafunzi wa sekondari na jamii nzima tuungane kwny hili
 
Wizi wa ccm ndo umetufksha apa tulipo .asanten kw kunisiklza
 
Tatizo ni kwamba nchi yetu inajua kupanga mambo lakini kutekeleza ni shida tu, maskini hana haki kwenye hii nchi. Angalia waliokosa mikopo ni watoto wa maskini na waliopata asilimia 100 ni watoto wa wa mapapa. Kuungana ni muhimu ila nafikiri ifike mahali hata wale waliopata mikopo waache kuingia darasani mpaka wenzao watakapopatiwa haki yao ya msingi ikiwezekana hii movement ipelekwe hata kwa wananchi watu waingie mtaani kuishinikiza nchi.
 

bro umenena me nakuunga mkono
 
Hivi kwani ofic zao ziko wapi hawa watu HESLB?!!!

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Tena wakija FFU tunatumia mafunzo ya JKT waliotufundisha..tuungane katika umoja hakuna la kushindikana
 

kweli apo umenena me mwenyewe npo kati ya miongon wasiopata mkopo mpaka muda huu nko tayar kufanya chochote ili nipate haki yangu maana roho inaniuma sana
 
Msijali wadau taarifa sahihi mwishoni mwa wiki au mwanzoni mwa wiki majina ya nyongeza walio kosa mkopo yatatoka tena msijali ukweli makini na net muhimu sana wadau
 
Msijali wadau taarifa sahihi mwishoni mwa wiki au mwanzoni mwa wiki majina ya nyongeza walio kosa mkopo yatatoka tena msijali ukweli makini na net muhimu sana wadau

mdau samahan tunaomba chanzo cha hii taarifa, mbona ikiwa hivyo itakua poa sana mdau maana saiv hali ni mbaya sana mdau
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…