Mliomshambulia January Makamba njooni mumpongeze baada ya hali ya umeme kutengemaa

Huo ni wajibu wake na wananchi wanahaki ya kulalama vitu visipokuwa sawa

Unataka tumpongeze kwani kaleta mageuzi ya umeme Bure🙃
amadala Tambua kuwa kiongozi akifanya vyema siyo dhambi kumpongeza na kumtia moyo,ndio maana ya hata uanzishaji wa tuzo mbalimbali Duniani ili kuwatia moyo wale wanaofanya vyema na kuleta mabadiliko chanya katika jamii na maeneo yao ya kazi
 
Thread ukiona tu unaiona sio real, January na Le Mutuz wanajianzishia thread na kujisifia hatare, na vijana wao wakichangia ni kusifu. hizi vitu vya ku feki ndio zimepoteza ladha za JF siku hizi.
 
Thread ukiona tu unaiona sio real, January na Le Mutuz wanajianzishia thread na kujisifia hatare, na vijana wao wakichangia ni kusifu. hizi vitu vya ku feki ndio zimepoteza ladha za JF siku hizi.
Kwani mh Makamba ndio ameandika hapa,Mimi Lucas Mwashambwa ndiye nimeandika
 
we si umetumwa kuandika wewe unashindwa kuandika thread inayoendana na wakati huu, gharama ya vitu na chakula vimepanda mara dufu january hii we unasifia
Acha mkulima Naye afaidike na jasho lake na siyo kuwa mtu wa kupata hasara kila mwaka
 
Hapana ndugu yangu Mimi siongelei habari za Urais Maana Rais wetu Ni mmoja ambaye Ni Dr Samia mpaka 2030 ndio tutaangalia Nani atatufaa Kuendeleza kazi ya kutukuka ya mh Rais wetu mpendwa mama Samia
Kizazi cha watu wa aina yako ndio 60% ya waafrika wote, ni kizazi batili kisicho jitambua. Mnatuchelewesha matakataka nyinyi
 
Tangu lini mke akapongezwa kwa kumpa unyumba mmewe?
 

Umeme umetengemaa wapi? Dar mgao upo kama kawaida, naongea na ww now kigamboni tayari washachukua umeme wao tangu saa 12 asubuh
 
Naomba kujua kama ulisharuhusiwa kutoka Milembe Hosp.???
 
Hapa tu sina umeme. Yaani nawaza nikikutana nae nikung'ute hata ngumi. Amezidi usanii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…