Mliomshambulia January Makamba njooni mumpongeze baada ya hali ya umeme kutengemaa

Kukatika kwa Umeme kulitokana na Hali ya ukame iliyokuwa imeikumba nchi yetu Kama ambavyo tulielezwa na mh Amiri Jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na Usalama mh Dr Mama Samia Suluhu Hassan
Kusema ukweli ni kitu kimoja. Kudanganya ni dhambi nyingine. Inaonyesha jinsi mtu anavyokosa confidence na kujaribu kukwepa uwajibikaji kwa dhamana aliyonayo.
Kipara hana uwezo wa kuwa kiongozi mkubwa. Ila kwa nafasi za kutumwa na wakubwa, anafaa. Tena akae kiti cha mbele. Ila sio yeye anaongoza mbele sisi wengine tunamfuata. Hana uwezo wala sifa hizo
 
Heri ungemsifia bro Geor pale kisongo hemani anaposambaza vijisenti, usingekosa hata 1 milion.

Kumsifu Makamba ni kujitangazia umaskini, acha mara moja.
 

Kwani hali ya umeme kuanza kutulia kwa mbali ni jitihada za January au mvua zinanyesha? Chawa unadhani kila mtu ni Chawa kama wewe?
 
Leo tumeshinda siku mzima hatuna umeme
Lucas natumai hauna matatizo ya akili
nahisi ni kipindi tu utakua sawa hapo tumsifie Nani aliekaa miaka Takriban mitano umeme haukatiki au huyu aliekaa mwaka mmoja na amekaa anatusumbua na umeme takriban miez sita Leo tumeshinda siku mzima hatuna umeme mpaka nashindwa kuelewa walisema tatizo mvua mbona zinanyesha na bado wanakata umeme unategemea Sisi watanzania tutaacha kuyaamini maneno ya magufuli aliekua anayasema wanawakatia umeme makusudi ili wauze majenereta
Hata kama unataka teuzi kupitia uchawa njoo taratibu asee usisifie upuuzi wa makamba na hanganya kwenye umeme
 
Jijini Mwanza Ilemela mgao kama kazi usitoe sifa za jumla bila utafiti wa kutosha.
 
Mikutano ya siasa ruksa sasa mjiandae kuyaeleza hayo kwa watu muone hali halisi
 
Risala yako sijaisoma ingenichosha tuu tulimsema kwasababu tulikua tunanyimwa haki yetu ambayo tunalipa wenyewe sasa apongezwe kwa kipi wakati hii ndo kawaida iliyotakiwa yaani tumpongeze kwa sababu umeme haukatiki basi we mwenzetu una tatizo ktk uelewa wako NIMEKUSHANGAA SANA
 
Brother Acha pumba mtu hapongezwi kwa kukamilisha majukumu yake ipasavyo mzee tunasema tu aongeze juhud tu zaidi
 
Brother Acha pumba mtu hapongezwi kwa kukamilisha majukumu yake ipasavyo mzee tunasema tu aongeze juhud tu zaidi
Wangapi wanalipwa mishahara na malupu lupu lakini wanashindwa kutimiza majukumu Yao,Sasa inapotokea mtu anatekeleza wajibu wake vizuri kwanini asipongezwe? Kwanini asitiwe moyo? Kwa Nini asiungwe mkono? Unafikiri walioanzishajlga tuzo kuwapa waliofanya vizuri katika majukumu Yao na sehemu zao za kazi walikuwa wajinga?
 
Kwani nafasi aliyopo Ni ndogo? Kwani huoni namna miradi ya umeme Inavyoendelea kupelekea vijijini kufungua fursa za kiuchumi hasa kwa vijana na akina mama?
 
Huku niliko na maeneo mengi tu hakuna kukatika katika kwa umeme Kama awali
 
Bwege nini? Umeme unatakiwa uwepo tuu kilasiku ukikosekana ndiyo tunashangaa ukiwepo ni normal hakuna cha kusifu hapo umeme unapaswa kuwepo kilasiku
 
Kwani yeye kafanya nini jipya?
kaleta mvua?
Mleta hoja wewe ni mpuuzi sana!
Kipindi kuna ukame unafikiri serikali ilikuwa imejaa chini kupiga magoti kuomba Mvua,hujuwi serikali yetu ilikuwa kazini kutafuta vyanzo vingine vya nishati
 
Kwani nafasi aliyopo Ni ndogo? Kwani huoni namna miradi ya umeme Inavyoendelea kupelekea vijijini kufungua fursa za kiuchumi hasa kwa vijana na akina mama?
Anafaa kuwa naibu..He is not creative at all. Ndio maana the challenges which occured, have exposed him mercilessly as a person incapable of handling big issues.
mahesabu hayadanganyi. Ingawa waafrika tunapenda sana kudanganyana. Na kuandika hivi sio kwamba namchukia Kipara....Hana uwezo na ni kweli hana uwezo. Ngoja siku mfanye majaribio, halafu mtajua nachosema
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…