Mliooa "boxer" mnaanika wapi?

Mama Mkwe akizikuta haitapendeza, au ukitembelewa na wageni wa heshima itakuaje.


Bora nianike chumbani to,tatizo lenu boxer mnazo 1 lazima mzianike juani "kauka nikuzae".
Mkuu ni kauka "nikuvae" [emoji28] [emoji28] [emoji28]
 
Kufunika kwa kanga labda za wanawake ,boxer hazina shida kuanikwa tu wazi maana nikama bukta au kaptula ndogo .Kwani vikaptula vya watoto wa kiume miaka miwli hadi minne mnaanika wapi? Naona vipo sawa tu na boxer
inategemea na umri wako na hadhi yako. Hiwezi kuwa na watoto wakubwa, umbo kama letu hilii ukaanika boxer tu hivi hivi! lazima uwe na staha kidogo hata mkwe wako asione!
 
Mm nimefunga kamba chumbani kwa hiyo naanika chumbani hewa nyingi tuu.
 
Nguo za ndani zinapaswa kuanikwa nje zikauke vzr ili kuepusha magonjwa kama fangasi na UTI. Ni mila potofu tu ndizo zinawafanya mshindwe kuanika nje na aibu za hovyo hovyo. Mm najianikia nje kwenye kamba
 
Ndio maana zinaitwa nguo za ndani maana yake siri sasa unapozianika nje ili watu wajue rangi za nguo zako ili weje mfano wengine wanawake michupi mikubwa kama ile ya ndondo cup unaanzaje kuianika nje tafuta sehemu nzuri ndani anika nguo zako unazifua cku moja zikikauka piga pasi weka kwenye kabati
 
Mungu wangu! Unaogopa kuanika boxer nje!? Kwan shida iko api mkuu
 
Mamaa!! Sasa unaogopa kuanika nje?? Hiyo kitu ukiifua unainika juan hakuna asievaa boxer acha ufala
 
Mimi boxer za mume wangu na vyupi vyangu huwa naanika nje kwenye jua .kwa nini nijitese .
 
Mbona huwa zinauzwa hadharani!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…