Mliopata mkopo wa Elimu ya juu mlitutambia sana

Mliopata mkopo wa Elimu ya juu mlitutambia sana

ntuchake

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2024
Posts
408
Reaction score
1,549
Nyie watu mliosomeshwa kwa mkopo wa serikali elimu ya juu mlikuwa mnatutambia sana sie tulionyimwa mkopo. Mlikua mnajiona wajanja wenyewe 😂😂 mmepata kazi umefika mda wa kulipa deni mnaanza kulia lia ooh mshahara hautoshi mara ooh wanakata sana.

Mlitegemea nani awalipie? Wakati mnatumia mliona raha wakati wa kulipa visingizio kibao!

Mtulie kama mnanyolewa mlipe deni la Serikali. Raha ya deni ni kulipa sio kulalamika 😂

Nasema hiviii mkome kuja kutujazia server JamiiForums hatuwezi kuwasaidia chochote kalalamikeni kwa mliokua mnatumia nao bumu! tupunzisheni na malalamiko yenu.

Soma Pia: Mngetumia nguvu za kuwapangia wanafunzi jinsi ya kutumia boom lao kuhakikisha wanaostahili wanapata mkopo 100% (au kusoma bure) tungewaona wa maana

Tulionyimwa mkopo tujuane katika huu uzi 🤗 huu ndo wakati wetu wa kutamba.
 
Back
Top Bottom