Mliwezaje kuinuka tena?

Mliwezaje kuinuka tena?

clearmind

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2013
Posts
813
Reaction score
1,913
Ningependa kufahamu, wengine mliwezaje kuinuka tena baada ya kuanguka kiuchumi? Mlitumia mbinu gani kuondoka katika hali ya ufukara uliokithiri, na ni nini kilichowasaidia kufanikisha hilo?

Mbona kwangu imekuwa tofauti sana?

Inaonekana kuisha miaka mitatu, bado nikiwa katika giza nene baada ya kuanguka, na kila juhudi ninayofanya inanipeleka nyuma zaidi.

Napambana kwa kila hali lakini hakuna kinachonipa matunda, moyo wangu unauma mno.

Mliwezaje?
 
Ningependa kufahamu, wengine mliwezaje kuinuka tena baada ya kuanguka kiuchumi? Mlitumia mbinu gani kuondoka katika hali ya ufukara uliokithiri, na ni nini kilichowasaidia kufanikisha hilo? Mbona kwangu imekuwa tofauti sana? Inaonekana kuisha miaka mitatu, bado nikiwa katika giza nene baada ya kuanguka, na kila juhudi ninayofanya inanipeleka nyuma zaidi. Napambana kwa kila hali lakini hakuna kinachonipa matunda, moyo wangu unauma mno. Mliwezaje?
Mkuu,

Pole sana. Shikilia sana network yako na ijenge zaidi bila kuchoka, halafu jijue wewe mwenyewe unaweza nini ujiongeze sana hapo, kisha, usione aibu kuomba msaada wa hali na mali pale unapoona una uhitaji.

Kuna mitihani mingine inaonekana migumu sana wakati unapoipitia, mpaka unaweza kufikiri vibaya, lakini ukiipita unaweza hata kucheka.

Miaka hii ya karibuni maisha yamekuwa magumu sana kwa watu wengi, lakini gangamala na jiongeze tu, yana mwisho yote haya.
 
Mkuu,

Pole sana. Shikilia sana network yako na ijenge zaidi bioa kuchoka, halafu jijue wewe mwenyewe unaweza nini ujiongeze sana hapo, kisha, usione aibu kuomba msaada wa haki na mali pale unapoona una uhitaji.

Kuna mitihani mingine inaonekana migumu sana wakati unapoipitia, mpaka unaweza kufikiri vibaya, lakini ukiipita unaweza hata kucheka.

Miaka hii ya karibuni maisha yamekuwa magumu sana kwa watu wengi, lakini gangamala na jiongeze tu, yana mwisho yote haya.
Asante sana ndugu yangu. Mungu akubariki sana.
 
Mkuu,

Pole sana. Shikilia sana network yako na ijenge zaidi bila kuchoka, halafu jijue wewe mwenyewe unaweza nini ujiongeze sana hapo, kisha, usione aibu kuomba msaada wa hali na mali pale unapoona una uhitaji.

Kuna mitihani mingine inaonekana migumu sana wakati unapoipitia, mpaka unaweza kufikiri vibaya, lakini ukiipita unaweza hata kucheka.

Miaka hii ya karibuni maisha yamekuwa magumu sana kwa watu wengi, lakini gangamala na jiongeze tu, yana mwisho yote haya.
Nilikuwa na network nzuri sana kabla ya kufikwa na hii Hali. Baada ya kuanguka, mazingira yamekuwa magumu mno. Hata ninapokwama hakuna wa kumtazama. Inaumiza mno.
 
Hiyo inatokea sana. Chukua hii kama nafasi ya kuwajua watu nani ni rafiki wa kweli na nani alikuwa na wewe wakati mambo yako yalikuwa mazuri tu.
 
Achana na mambo haya kama unafanya betting, Forex, wanawake, starehe zisizo za lazima.
Pesa yoyote ambayo itapita mikononi mwako hata kama ni buku hakikisha inaenda kwenye msosi au kodi ya nyumba, katika kipindi kama hiki usikubali kupoteza pesa yako kirahisi.
Jikite kutafuta kazi ya kipato endelevu usidharau kazi hizi ndogo ndogo wew fanya pia usiishi kwa kuangalia watu watanionaje mm msomi au nilikuwa mtu fulani huko nyuma.
La mwisho penda kwenda kanisani au msikitini huko utapata Amani ya roho utajihisi somehow ukofree.
Nimeishi hivyo nikiwa na hali mbaya ya kifedha jijini dar es salaam kwa zaidi ya miaka 4 tena nikiwa na familia ila hizo njia zimenisaidia sana hadi kupata siku napata kazi ya maana.
 
You are like me man! And I stood up again!
Kwanza niliacha maisha ya zamani, (starehe zote) na ni baada ya kugundua sikua na marafiki Bali nilikua na parasites ambao baada ya Hali ngumu ya kupoteza Kila kitu waligeuka maadui na kunisema vibaya. Nilijitenga nao kwanza.

Kurudi kanisani, kanisani hasa ukipata kanisa ambalo halihubiri kwa vitisho l, kanisa ambalo linafundisha kanuni za maisha, na thamani ya mwanadamu. Katika hili hakika utapata amani ya moyo, akili na Roho na kiyatazama maisha kwa matumaini makubwa. Utakumbuka agano la Mungu na wewe, utakumbuka your purpose!
Utakua na sababu ya kuchagua new circle ya mtazamo mpya na mtazamo chanya.

Mungu akisha kukusaidia kujutengeneza hakika unasimama upya na unaenda hatua kubwa zaidi! Kila unachokifanya utatambua thamani yake na utailinda!
 
Ningependa kufahamu, wengine mliwezaje kuinuka tena baada ya kuanguka kiuchumi? Mlitumia mbinu gani kuondoka katika hali ya ufukara uliokithiri, na ni nini kilichowasaidia kufanikisha hilo?

Mbona kwangu imekuwa tofauti sana?

Inaonekana kuisha miaka mitatu, bado nikiwa katika giza nene baada ya kuanguka, na kila juhudi ninayofanya inanipeleka nyuma zaidi.

Napambana kwa kila hali lakini hakuna kinachonipa matunda, moyo wangu unauma mno.

Mliwezaje?
Upo katika mapito. Ni hali ngumu sana mimi nilikaa huko miaka minne. Giza nene na hofu ya maisha vilinizunguka.

Kinachotakiwa ni kusimama imara. Usikubali kudhoofishwa afya yako, maono yako, morali yako au kuondoka kwenye ndoto na makusudio yako.

Kumbuka ni mapito tu hayo, yanapita kama upepo na ni majaribu au mtihani na unapaswa kufaulu.

Angalia ni wapi ulikosea. Rekekebisha.

Anza upya. Sio lazima ufanikiwe kwa kutumia njia unazozijua au ulizozoea. Badili gia. Hata ikibidi badili mazingira unayoishi,. Hama hapo ulipo.

Ulimwengu ni mpana na yapo yasiyo dhahiri machoni petu lakini yapo na yanatuathiri bila sisi kujua ni kwa namna gani. Uchawi na hila za wanadamu vipo! Hakikisha unaondokana na madhila haya.

Anza kuchangamkia kurudi kwako kwenye njia ya matumaini ni haki yako kufanikiwa! Kama wewe unaamini katika Mungu ni wakati wa kuzitafuta njia zake. Omba sana, wakati huo huo fanya kazi kwa bidii.
 
1.Jiweke karibu na Mungu
2.Achana na anasa hasa wanawake
3.Piga chini cycle yako ya watu wako wa zamani ambao hawana msaada kwako ktk kipindi hiki kigumu.
4.usije ukadanganyika kwenda kwa waganga ndio utapotea mazima.
5.kila sent unayoipata itumie kwa matumizi muhimu ya familia hasa chakula,rent na ada.
6.Fanya kazi yoyote halali inayokuja mbele yako bila kujali watu wanaokujua watasemaje.
 
Upo katika mapito. Ni hali ngumu sana mimi nilikaa huko miaka minne. Giza nene na hofu ya maisha vilinizunguka.

Kinachotakiwa ni kusimama imara. Usikubali kudhoofishwa afya yako, maono yako, morali yako au kuondoka kwenye ndoto na makusudio yako.

Kumbuka ni mapito tu hayo, yanapita kama upepo na ni majaribu au mtihani na unapaswa kufaulu.

Angalia ni wapi ulikosea. Rekekebisha.

Anza upya. Sio lazima ufanikiwe kwa kutumia njia unazozijua au ulizozoea. Badili gia. Hata ikibidi badili mazingira unayoishi,. Hama hapo ulipo.

Ulimwengu ni mpana na yapo yasiyo dhahiri machoni petu lakini yapo na yanatuathiri bila sisi kujua ni kwa namna gani. Uchawi na hila za wanadamu vipo! Hakikisha unaondokana na madhila haya.

Anza kuchangamkia kurudi kwako kwenye njia ya matumaini ni haki yako kufanikiwa! Kama wewe unaamini katika Mungu ni wakati wa kuzitafuta njia zake. Omba sana, wakati huo huo fanya kazi kwa bidii.
Amina, Asante sana
 
Back
Top Bottom