Mkuu,Ningependa kufahamu, wengine mliwezaje kuinuka tena baada ya kuanguka kiuchumi? Mlitumia mbinu gani kuondoka katika hali ya ufukara uliokithiri, na ni nini kilichowasaidia kufanikisha hilo? Mbona kwangu imekuwa tofauti sana? Inaonekana kuisha miaka mitatu, bado nikiwa katika giza nene baada ya kuanguka, na kila juhudi ninayofanya inanipeleka nyuma zaidi. Napambana kwa kila hali lakini hakuna kinachonipa matunda, moyo wangu unauma mno. Mliwezaje?
Asante sana ndugu yangu. Mungu akubariki sana.Mkuu,
Pole sana. Shikilia sana network yako na ijenge zaidi bioa kuchoka, halafu jijue wewe mwenyewe unaweza nini ujiongeze sana hapo, kisha, usione aibu kuomba msaada wa haki na mali pale unapoona una uhitaji.
Kuna mitihani mingine inaonekana migumu sana wakati unapoipitia, mpaka unaweza kufikiri vibaya, lakini ukiipita unaweza hata kucheka.
Miaka hii ya karibuni maisha yamekuwa magumu sana kwa watu wengi, lakini gangamala na jiongeze tu, yana mwisho yote haya.
Nilikuwa na network nzuri sana kabla ya kufikwa na hii Hali. Baada ya kuanguka, mazingira yamekuwa magumu mno. Hata ninapokwama hakuna wa kumtazama. Inaumiza mno.Mkuu,
Pole sana. Shikilia sana network yako na ijenge zaidi bila kuchoka, halafu jijue wewe mwenyewe unaweza nini ujiongeze sana hapo, kisha, usione aibu kuomba msaada wa hali na mali pale unapoona una uhitaji.
Kuna mitihani mingine inaonekana migumu sana wakati unapoipitia, mpaka unaweza kufikiri vibaya, lakini ukiipita unaweza hata kucheka.
Miaka hii ya karibuni maisha yamekuwa magumu sana kwa watu wengi, lakini gangamala na jiongeze tu, yana mwisho yote haya.
Amina!Pole sana yapokee matokeo anza upya taratibu bila kuchoka jaribu kila siku inayoisha iwe bora zaidi katika upambanaji.
Hiyo inatokea sana. Chukua hii kama nafasi ya kuwajua watu nani ni rafiki wa kweli na nani alikuwa na wewe wakati mambo yako yalikuwa mazuri tu.Nilikuwa na network nzuri sana kabla ya kufikwa na hii Hali. Baada ya kuanguka, mazingira yamekuwa magumu mno. Hata ninapokwama hakuna wa kumtazama. Inaumiza mno.
Asante sana ndugu yangu. Maumivu ni makali mno.Pole sana mkuu naelewa hali unayopitia.
Yatapita hakuna lisilokuwa na mwisho, usichoke kupambana na usikate tamaa.Asante sana ndugu yangu. Maumivu ni makali mno.
You are like me man! And I stood up again!Achana na mambo haya kama unafanya betting, Forex, wanawake, starehe zisizo za lazima.
Pesa yoyote ambayo itapita mikononi mwako hata kama ni buku hakikisha inaenda kwenye msosi au kodi ya nyumba, katika kipindi kama hiki usikubali kupoteza pesa yako kirahisi.
Jikite kutafuta kazi ya kipato endelevu usidharau kazi hizi ndogo ndogo wew fanya pia usiishi kwa kuangalia watu watanionaje mm msomi au nilikuwa mtu fulani huko nyuma.
La mwisho penda kwenda kanisani au msikitini huko utapata Amani ya roho utajihisi somehow ukofree.
Nimeishi hivyo nikiwa na hali mbaya ya kifedha jijini dar es salaam kwa zaidi ya miaka 4 tena nikiwa na familia ila hizo njia zimenisaidia sana hadi kupata siku napata kazi ya maana.
Upo katika mapito. Ni hali ngumu sana mimi nilikaa huko miaka minne. Giza nene na hofu ya maisha vilinizunguka.Ningependa kufahamu, wengine mliwezaje kuinuka tena baada ya kuanguka kiuchumi? Mlitumia mbinu gani kuondoka katika hali ya ufukara uliokithiri, na ni nini kilichowasaidia kufanikisha hilo?
Mbona kwangu imekuwa tofauti sana?
Inaonekana kuisha miaka mitatu, bado nikiwa katika giza nene baada ya kuanguka, na kila juhudi ninayofanya inanipeleka nyuma zaidi.
Napambana kwa kila hali lakini hakuna kinachonipa matunda, moyo wangu unauma mno.
Mliwezaje?
Relax,fanya Mambo yako ukiwa na utulivu wa moyo la sivyo utavuruga kilakituAsante sana ndugu yangu. Maumivu ni makali mno.
Amina, Asante sanaUpo katika mapito. Ni hali ngumu sana mimi nilikaa huko miaka minne. Giza nene na hofu ya maisha vilinizunguka.
Kinachotakiwa ni kusimama imara. Usikubali kudhoofishwa afya yako, maono yako, morali yako au kuondoka kwenye ndoto na makusudio yako.
Kumbuka ni mapito tu hayo, yanapita kama upepo na ni majaribu au mtihani na unapaswa kufaulu.
Angalia ni wapi ulikosea. Rekekebisha.
Anza upya. Sio lazima ufanikiwe kwa kutumia njia unazozijua au ulizozoea. Badili gia. Hata ikibidi badili mazingira unayoishi,. Hama hapo ulipo.
Ulimwengu ni mpana na yapo yasiyo dhahiri machoni petu lakini yapo na yanatuathiri bila sisi kujua ni kwa namna gani. Uchawi na hila za wanadamu vipo! Hakikisha unaondokana na madhila haya.
Anza kuchangamkia kurudi kwako kwenye njia ya matumaini ni haki yako kufanikiwa! Kama wewe unaamini katika Mungu ni wakati wa kuzitafuta njia zake. Omba sana, wakati huo huo fanya kazi kwa bidii.