Mmea Wa Hofu

La Quica

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2017
Posts
1,009
Reaction score
2,315
Mwenye gari hili aliamka asubuhi na kung'amua mzingiro huo mweupe kwa usafiri wake.

Kwa hofu ya dhahiri, aliacha kulitumia akawa anaenda kwa taxi kazini kwake. Muungwana huyu alimuita Fundi Makenika asaidie kulivuta, lakini mwigo wa hofu ukamwingia fundi nae akatokomea baada ya kuona mzingiro huo.

Sasa, akitoka kazini anakuta Mwanae anacheza cheza kwenye duara hilo. Baba alimbwatukia si kitoto, lakini mwana huyo mdogo akamwambia "Baba ni mimi nimezungushia hapa. Mama alinipa unga wa mahindi uliokwisha muda wake kuumwaga. Nikazungushia hapa ili niwe nacheza kwenye duara."

Hadi unaposoma ujumbe huu amini kwamba, yule Bwa'Mdogo anakula kichapo.
 
Huna kazi nyingine?
[emoji16][emoji16][emoji16] Maisha yangu yanaenda kupitia biashara za mtandao sasa ukiona mtu mtandaoni usidhani hana kazi.

Simu/Computer kwangu ni kama maji mwilini kila muda nalazimika kuwa nayo hadi saa 6 usiku..
 
Kwahiyo bishara yako ni kuchangia kila uzi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…