Mmea wa kukuza sehemu za siri wagundulika

Ndibalema

JF-Expert Member
Joined
Apr 26, 2008
Posts
10,955
Reaction score
4,656
Sasa unaweza kuachana na dawa hizo za Kichina, baada ya kugundulika mmea wenye uwezo wa kukuza makalio, matiti, pamoja na kurefusha uume.
Taarifa za kiutafiti zinautaja mti huo kwa jina la Mvunge, ukiwa na uwezo wa kukuza makalio, matiti na kurefusha uume.


Kaimu Msajili wa Tiba Asili na Tiba Mbadala nchini, Dk Naomi Mpemba anasema kuwa mmea huo ambao huwa ni mti mkubwa upo na kwamba una uwezo mkubwa wa kukuza maumbile hayo.


Anabainisha kuwa mmea huo ambao hukua na kuwa mti mkubwa huzaa matunda yanayotumika kama dawa na unapatikana wilayani Korogwe Mkoa wa Tanga, Pwani, Mbeya, Morogoro na baadhi ya mikoa nchini.


“Tulifuatilia na kutambua kuwa mti huo upo maeneo hayo na unatumiwa zaidi na waganga, hata picha za mti huo tunazo,” anasema Dk Mpemba na kuongeza:


“Jina jingine unaitwa Miegeya, mara nyingi unastawi katika maeneo yenye ardhi ya unyevunyevu, una tabia ya kustawi kama Mwembe na matunda yake huonekana kufanana na Mbuyu.”


Hata hivyo, anasema kuwa asilimia kubwa ya waganga wa tiba asili na tiba mbadala wanaotumia dawa hiyo ni wale wasiokuwa na usajili kutoka baraza hilo, hivyo kufanya huduma hizo kinyume cha utaratibu.


“Kwa mujibu wa masharti yaliyopo katika agizo la Serikali kwa waganga hao, miiko, maadili na utendaji wa kazi zao umeelekeza kuwepo na usiri na kuaminiwa, kwa hiyo sisi tunaamini wanaojitangaza kutibu mambo hayo ni matapeli,”anasema Dk Mpemba.



Source: Mmea wa kukuza sehemu za siri wagundulika - Kitaifa - mwananchi.co.tz
 

Attachments

  • mtiii.jpg
    23.8 KB · Views: 1,035
Kuongeza ukubwa wa maumbile bila kujua uwezo wako wa mishipa ya damu inaweza kukusababishia uwe na joka la kibisa dadeek ...shortly stop to poison u'r self and then eat da nature food kwishney kitu mwanzo mwisho ...anyway thnx 4 info mkuu.
 
huo naujua tangu utoto,. wakati nikiwa mdogo nilipokuwa na bibi yangu tukiwa shamba bibi yangu siku zote alikua ananiambia.ila alikuwa anasema kama ni mwanaume lazima nichanje kwenye sehemu za siri,kwa mwanamke lazima achanje kwenye maziwa habari za makalio sijawahi kusikia.,[hiyo ilikuwa mwaka 1980]kweli uzee dawa
 
Huu mti upo shambani kwa bibi yangu tokea nikiwa mdogo.
Kama kuna mseti tuwasiliane nianze kusuply dozi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…