Mmiliki wa jengo la Kariakoo tayari amekamatwa. Kwanini anafichwa?

Mmiliki wa jengo la Kariakoo tayari amekamatwa. Kwanini anafichwa?

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Wakuu,

Ukurasa wa X wa East Africa TV wamepost kuonesha kuwa mmiliki wa jengo la Kariakoo amekamtwa

Msemaji Mkuu wa Serikali, Thobias Makoba, ametangaza kuwa mmoja wa wamiliki wa jengo lililoporomoka katika eneo la Kariakoo, na kusababisha vifo vya watu 29 pamoja na majeruhi kadhaa, tayari amekamatwa.

Makoba alibainisha kuwa taratibu za kisheria dhidi ya mtuhumiwa huyo zinaendelea, huku akisisitiza kuwa serikali haitasita kuchukua hatua kali kwa yeyote atakayebainika kuwa na makosa yanayohusiana na tukio hilo.

Kkoo.png

Source: EastAfrica Radio
 
Hapo kuna macontawa wa mjini wanaenda kwenye mali wanamwambia kama pumzi yako ndogo nipe mimi umiliki wa Hilo jengo niingie matatizoni ila utanipooza issue ikiisha unarud kwenye mali yako
 
Hapo kuna macontawa wa mjini wanaenda kwenye mali wanamwambia kama pumzi yako ndogo nipe mimi umiliki wa Hilo jengo niingie matatizoni ila utanipooza issue ikiisha unarud kwenye mali yako
Kabisa mkuu, mjini kuna mengi yenye hoja na viroja ila mwisho wa siku watu wanaishi na kutengeneza pesa maisha yanaendelea. Ukishakuwa na pesa ukiwa mahabusu polisi au magereza unaishi kama mfalme.
 
Hongera Serikali

Nakuchukia tu.. "Nilidhani tatizo kukuchukia"

images.jpg
 
Kama kawaida yetu..

Tumeshasahau mpaka janga lingine lije ndio tuanze kufukua nyuzi humu.

Mwezi mzima unaenda kufika sarakasi na kelele zote zitapita hata ile kampeni ya kukagua majengo yote haitofanywa hadi lingine lidondoke.
 
Back
Top Bottom