Mmiliki wa kampala international university hafai

KIGENE

JF-Expert Member
Joined
Jan 22, 2011
Posts
1,552
Reaction score
813
Mmiliki wa KIU Bassajabalaba ni mfanyabiashara anayeendesha shuguri zake kwa njia za kifisadi na zenye utata.
Pamoja na biashara mbalimbali alizopata kuzifanya alikuwa ni muuzaji wa ngozi za wanyama (raw hides) nchi za nje, alijipatia mikopo mikubwa kutoka benki hili kufanikisha biashara hizo.
Lakini Bassajabalaba hakuweza kurejesha fedha za benki na halimanusura afilisiwe kama isingekuwa rafiki yake rais Mseveni kuingilia kati.
Itakumbukwa kuwa Bassajabalaba anatokea sehemu moja na Museveni ni tu wake wa karibu na alikuwa anafadhili chama cha Mseveni kama kichaka cha kuficha madhambi yake.
Mtu huyohuyo alikuwa na makesi kibao mahakamani yanayohusiana na kujipatia mali za baraza la waislamu kinyume na sheria baada ya kula njama na viongozi wa baraza hilo.
Bassajabalaba hakuishia hapo alienda mbali zaidi na kuingia mikataba ya kifasadi na Halmashauri ya jiji la Kampala ya kuendesha masoko ya Kampala.
Baadae mikataba ikabadilishwa kinyemela nakumwezesha kuwa mmiliki kamili wa masoko hayo, kwa bahati nzuri wafanyabiashara katika masoko hayo wakawa ngangari nakusababisha vurugu kubwa siku ya makabidhiano ambapo magari yalichomwa moto na mali nyingi kuharibiwa, na safari hii ilikuwa ni Mseveni kuingilia kati na kufutilia mbali mikataba ya kimangumashi.
Hata chuo chake KIU Kampala main campus kilianza kwa misukosuko kati yake na mamlaka zinazousika na vyuo vya elime ya juu,baadhi ya matatizo ilikuwa ni vitivo kutokidhi viwango kutokuwa na wahadhiri wakutosha na wakati mwingine viwango vyao kuwa chini.
Lakini kwa ukaribu wake na rais ikawa ni funika kombe mwanaharamu apite.
Kwa ufupi huyo ndie mwenye vyuo vya KIU hata hapa kwetu naona mambo ni yale yale mara waadhiri hawalipwi mishahara kwa miezi tisa mara wanachuo kulazimishwa kulipia ada kwa US Dollar.
Mamlaka zinazohusika hazina budi kumfuatilia huyu bwana kwa karibu vinginevyo wa Tanzania tutaula wa chuya, kwa jeuri anayoonyesha uenda amekuja na kimemo toka kwa Mseveni kwenda kwa mkuu wa kaya.

 
Yaani kwa kuonyesha msisitizo hata maanndishi yako umeyaandika kwa wino mweuuusi,kama waganda wengi walivyo!!
 
Sasa kati ya huyu aliyewekeza katika nchi ya africa kwa manufaa ya wengi vs. wanaoweka pesa uswisi nani zaidi?
 
Sasa kati ya huyu aliyewekeza katika nchi ya africa kwa manufaa ya wengi vs. wanaoweka pesa uswisi nani zaidi?

Mara kumi ya uyu aliyewekeza kwenye nchi yake, kuliko hawa mafisadi we2 wanapora hela za wabongo na kuzificha kwenye account za nje na kuziondoa kwenye mzunguko wa pesa ndan ya nchi!
 
wote wahuni..uwepo wa wabaya zaidi yako haukufanyi ww kuwa mwema
 
isambe;5329871]Yaani kwa kuonyesha msisitizo hata maanndishi yako umeyaandika kwa wino mweuuusi,kama waganda wengi walivyo!!
Hapo sijakuelewa mkuu unfortunately mi si Mganda ni Mtanzania per se
 
By Chimbuvu
Sasa kati ya huyu aliyewekeza katika nchi ya africa kwa manufaa ya wengi vs. wanaoweka pesa uswisi nani zaidi?
Hapa hoja si mwekezaji mwafrica au taifa lingine,tunachokihitaji ni mwekezaji makini kwa maslahi yake na sisi wenyewe sio bora mwekezaji hata kama hatakuwa na manufaa kwetu.
Just imagine mwekezaji anayeshindwa kuwalipa mishahara wahadiri zaidi ya thelasini kwa kipindi cha miezi tisa,na baada ya vuta nikuvute anaamua kuwatimua kazi hata bila kuwalipa, hapo hapo anawaleta wahadhiri wengine toka Uganda kuchukua nafasi za wa Tanzania.
Mwekezaji kama huyu mimi naona hafai,msemo wa kichina unasema usijari rangi ya paka ilimradi anakamata panya.

 
:target:kwa nn ukubar kufanya kaz kw muda mref ivo bila mshahara? walikuwa wanaishije?
 
:target:kwa nn ukubar kufanya kaz kw muda mref ivo bila mshahara? walikuwa wanaishije?

Kwa kupiga vizinga/virungu .......mtoa mada naona kaongeza chumvi siyo miezi 9 ni miezi 3.
 
Napongeza suala la huyu mganda kuwekeza kwetu Tanzania hasa kwenye eneo muhimu la elimu.

Lakini uwekezaji usioangalia viwango vya ubora wa huduma na maslahi ya wanachi huenda ukawa na madhara makubwa sana.

Licha ya kuwacheleweshea kuwalipa mishahara wafanyakazi, hawalipi kwa akaunti zao za benki, baadhi ya wafanyakazi wanaenda kulipwa mkononi kama vibarua. Sasa sijui kama kuna mambo ya PAYE au NSSF hapo.
 
Maprosoo;Kwa kupiga vizinga/virungu .......mtoa mada naona kaongeza chumvi siyo miezi 9 ni miezi 3.
Chuo cha Kimataifa Kampala (Kiu), kimewatimua wahadhiri wake 35 kwa madai ya utovu wa nidhamu ikiwamo kutohudhuria darasani kwa wiki tatu.

Hata hivyo, wahadhiri hao wamedai kwamba kufukuzwa kwao kumesababishwa na kudai mishahara yao ya miezi tisa.

Mkurugenzi wa Kiu, Hassan Bassaja, alisema wahadhiri hao wamekiuka sheria za msingi za chuo hicho kwa kugoma kuingia darasani kwa wiki tatu mfululizo.

"Nimeamua kuwafukuza kazi wahadhiri hao kwa kuwa wamekiuka sheria zetu kwa kutoingia darasani kufundisha, kitu ambacho kimesababisha kuahirishwa mitihani kwa wanachuo mpaka Januari, mwakani," alisema Bassaja.

Hata hivyo, mmoja wa wahadhiri hao ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini, aliliiambia NIPASHE kuwa kufukuzwa kwao kumechangiwa na kuidai menejimenti ya chuo mishahara yao ya miezi tisa.

Alisema walilazimika kutoingia darasani kwa lengo la kuishinikiza menejimenti iwalipe mishahara yao hiyo lakini uongozi imeamua kuwafukuza kazi.

"Tumefanya kazi kwa miezi tisa mfululizo bila kulipwa mishahara yetu na kila tukifikisha malalamiko yetu kwa Mkurugenzi amekuwa akiyapuuza na ndipo tulipoamua kugoma kufundisha," alisema mhadhiri huyo.

Hata hivyo, Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU), Profesa Sifuni Mchome, alisema wahadhiri hao lazima walipwe mishahara yao na suala la kuwafukuza kazi ni jambo tofauti kabisa.

"Walipwe mishahara yao kisha suala la kuwafukuza kazi litaangaliwa kwa undani zaidi. Maana hapa ni kama kuanzisha suala lingine wakati la awali bado halijashughulikiwa," alisema Profesa Mchome

Aidha, imedaiwa kuwa tayari uongozi wa chuo hicho umewaleta wahadhiri wengine 30 kutoka nchini Uganda kuchukua nafasi za wahadhiri waliofukuzwa kazi.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick, amemuagiza Afisa Elimu wa Mkoa, Raymond Mapunda, kufuatilia suala hilo.

Sakick amemtaka pia Afisa Elimu Mkoa wa Dar es Salaam, kulifikisha suala hilo Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi pamoja na TCU.

Hata hivyo, Afisa Elimu mkoani Dar es Salaam, alisema tayari amewasilisha TCU malalamiko ya wahadhiri pamoja na wanafunzi wa chuo hicho na kuhakikishiwa kuwa suala hilo litafanyiwa kazi ipasavyo.


CHANZO: NIPASHE
 
hakuna cha ubora ktk ufisad,lazima huyu jamaa achunguzwe..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…