Mmiliki wa kituo cha mafuta kufikishwa mahakamani kwa uhujumu uchumi

Mmiliki wa kituo cha mafuta kufikishwa mahakamani kwa uhujumu uchumi

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa wilayani Simanjiro mkoani Manyara kwa kushirikiana na ofisi ya Taifa ya mashtaka mnamo tarehe 22/06/2020 itamfikisha katika mahakama ya wilaya ya Simanjiro mmiliki wa kituo cha mafuta Simon Lemeya kilichopo Wilaya ya Simanjiro Simon Lemeya Tukai.

Lemeya atafikishwa mahakamani kwa kughushi matumizi ya nyaraka kudanganya na kuisababishia serikali hasara ya sh. milioni tano laki sita na elfu tisa (5,609,000) Kinyume cha Aya ya 10(1) jedwali la kwanza, kifungu cha 57(1) na 60(2) sheria ya uhujumu uchumi Cap 200 marejeo ya 2002.

Wengine waliounganishwa na Lemeya ni Ezekiel Fabiani Mayumba ambaye alikuwa Afisa afya na mratibu wa chanjo ya mama na mtoto wilayani Simanjiro na Ally Sadick Mnkeni na Simaloi Baby Lemeya ambao ni wafanyakazi vituo vya mafuta Simanjiro.

Uchunguzi wa TAKUKURU ulibaini kuwa mnamo mwaka 2014 walighushi nyaraka na kufanya ubadhilifu wa fedha za chanjo ya kitaifa ya Rubella na surua na kuisababishia hasara serikali ya sh. milioni tano laki sita na elfu tisa.
 

Attachments

Huu ni upumbavu. Yani milioni 5 unahujumu Uchumi? Si wamuambie alipe
 
Huu ni upumbavu. Yani milioni 5 unahujumu Uchumi? Si wamuambie alipe
Utajiri hauji kirahisi mkuu ndio maana watu wengi ni maskini.

Matajiri wana Siri nyingi ambazo hawawezi kusema, wanaua, wanadhurumu, wanakwepa kodi, wanahujumu, wanafanya biashara haramu, wanatoa kafara.

Sikatai wapo wengine wenye utajiri halali ila ni wachache sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom