Mmiliki wa nyumba ya kulala wageni akamatwa na kichwa cha albino

Mmiliki wa nyumba ya kulala wageni akamatwa na kichwa cha albino

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
[TABLE="width: 491"]
[TR="bgcolor: #E1E1E1"]
[TD]JAMES ISAME [50] mmiliki wa nyumba ya kulala wageni iitwayo Bongo Star Lodge iliyopo Kawe Ukwamani jijini Dar es Salaam, amekamatwa kwa kukutwa na kichwa cha binadamu kinachosadikiwa kuwa ni cha mlemavu wa ngozi [ablino]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 3"]Kufuatia hiyo Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni linamshikilia kutoa maelezo kuhusiana na tukio hilo

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela amesema mfanyabiashara huyo alikamatwa juzi majira ya saa 2:45 usiku baada ya wasamaria wema kutoa taarifa kuhusiana na tukio hilo

Kamanda Kenyela amesema mara baada ya taarifa hiyo kutolewa askari polisi walifika mahali hapo kwa ajili ya upekuzi katika nyumba hiyo ya kulala wageni iliyoambatana na baa

Amesema, walifanikiwa kukuta kichwa hicho cha binadamu kikiwa kimewekwa juu ya ukuta wa choo kikiwa kimevingirishwa katika mfuko wa rambo

“Ni kweli tumekikuta kichwa hicho kikiwa kimening’inizwa ukuta wa chooni,na tulikigundua kuwa ni cha binadamu baada ya kuona nywele na meno”

Kamanda Kenyela alizidi kufafanua kuwa katika uchunguzi walioufanya walibaini kichwa hicho kilikuwa ni cha mtoto ambacho bado hawajabaini ni cha jinsia gani

Hata hivyo Kamanda Kenyela alisema uchunguzi wa tukio hilo bado unaendelea

Mmiliki wa nyumba ya kulala wageni akamatwa na kichwa cha albino[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Imekaa kama jamaa alitegewa...na huenda wategaji walifukua maiti na siyo kuua...ndio maana hata utambuzi wa jinsia ulikuwa mgumu
 
tego hilo huwezi kaa na kicha cha bin adam ,labda ingekuwa kiungo. kingine
 
Back
Top Bottom