Mmmh!....HII SASA IMEZIDI; YAANI HATA IKULU INATUMIA "@YAHOO.COM" ??!!!

Kwanini watu wa JF tusijitolee kulipia Dedicated Server ya Ikulu kama mchango wetu?

Loo!!! mtatuua na michango kila kukicha, Mara ujenzi wa shule, Madawati, Dawa,Pesa za mgambo,Usafi wa mtaa,Mafuta ya mwenge,ujenzi wa barabara ya kijiji etc, wananchi tumechoka mbaya halafu tumwage maji baharini? hii ni sawa na Chenge kuomba nauli ya kwenda Bariadi
 
Steve D,

Tatizo la "wajanja" si kutaka 10%, ni machoism na ushindani wa kijinga wa Wanasiasa na Watendaji wa Tanzania ambao kila mmoja wao ni mjuaji na anataka awe na kauli ya mwisho na sauti kubwa!

Look at the CCM crisis brewing, kila mtu anaropoka vyake!
 

Ni afadhari kutumia hiyo ya yahoo. Maana wakifungua ya kwao unaweza kuambiwa inatumia shilingi bilioni moja kwa mwezi. Kurugenzi ya mawasiliano ikulu ni kama idara ya propaganda haina kazi ya maana na kuifanya iwepo. Idara ya habari maelezo inatosha sana
 

Huu ni mzaha na ni hatari!! Usalama wa taifa uko wapi?
 



Hodi hodi?
@yahoo.com? 😡
Rais ikulu wanafanyaje kazi?
Au bado kuna mesenja kibao wa kupeleka mafaili hapo?
internal communication ikoje?
calendar, tasks, na privacy ikoje?
Au labda wanayo internal email server.

Wanatakiwa wachukue hatua za haraka, ndiyo maana mambo mengi hayaendi kwa kasi mpya. No follow ups - where is share point kwa serikali yetu?
Maana kuwa na email server siyo kazi yake ni kutuma na kupokea emails tu;​
 
with this world of TEKNOHAMA kama ikulu ndo ilivyo basi hatuendi popote. hata usalama wa taifa uko shakani. VERY MUCH disappointed.
 
Jamaa wa Ikulu wanadai kwamba hiyo ya yahoo inapatikana kirahisi wakati wowote na wakiwa mahali popote duniani.


Bwahahahaha... Hahahahah!
Oh lord, what a shame.




Hili ni tatizo kubwa hata kuwa kikwazo kwenye juhudi za watu wa IT. Kuna fikra kwamba huyu kazi yake ni ku-fix computer and printers problems; hapo mtu unakuwa under-utilized kwa maana ya kwamba wakati mwingine unapewa kazi nyepesi ambazo zingetakiwa kufanywa na secretary.

Hali inaweza kuwa tofauti sehemu nyingine, kudhani kwamba mtu wa IT anaweza kufanya kila kitu. Blunders hufanyika kwenye ku-recruit IT staff bila shaka. Kuna post inayo-relate na hii issue, imeandikwa na David Stanley.





.
 
Wataalamu wangeachiwa wafanye kazi yao si kuingiza siasa kwenye shughuli za kitaalamu. naungana na lazydogy-Kuna fikra kwamba huyu kazi yake ni ku-fix computer and printers problems; hapo mtu unakuwa under-utilized kwa maana ya kwamba wakati mwingine unapewa kazi nyepesi ambazo zingetakiwa kufanywa na secretary.

Maana watu wengi wanajua computer ni kuchapa na kuprint!!!!!!!!!
 
Kwanini watu wa JF tusijitolee kulipia Dedicated Server ya Ikulu kama mchango wetu?

Kwa kazi gani inayofanyika hapo Ikulu? Usanii, utapeli na kunyima wananchi haki zao? Sioni cha kushangaza. Hapo ikulu kumejaa wasanii, matapeli, na wakandamizaji. Worst than 419 scam.
 

Asante sana wadau kwa kuchangia mjadala huu kwa kweli mie niliguswa sana na hali hiyo,japo samahani kwa kupotea kidogo nilibanwa na kazi fulani.Sijui kama hawa bwana wanasikia au kusoma hizi comments zetu, maana sawa kutumia hiyo @yahoocom sio mbaya labda inawasaidia mawasiliano, lakini kwa taaisis kama serikali tena ikulu,aaahh hapana hili halikubaliki.Kutumia anwani hiyo ya yahoo ni kuruhusu phishing kiurahisi,cybersquatting nk.Mbali ya hapo wale jamaa ambao hutuma e-mail kama hizi hapa chini:

ni rahisi sana kutumia opportunity kama hiyo kuwaibia watu sema tushukuru hatuna watanzania wengi macrooks kwenye IT(IT misuse) otherwise hali ingekuwa ngumu kweli kweli.
Kauli kwamba eti @yahoo inapatikana kirahisi wakiwa nje ya nchi sio kweli,huku ni kitania fani ya IT,kama sisi wengine tu blogu zetu zinapatikana popote duniani na mtu anaweza kuwasiliana nasi itakuwa wao?No,i this issue something is wrong somewhere,something must be done to get rid of this situation.
 

SteveD
You have said it all.Big Up! wawe wanakuja kusoma humu.
 

Hili la IKULU sasa linatuthibitishia aibu hii ambayo marekani wameamua kutudhalilisha nao mchana kweupeeeeeeeeeeee

source:http://www.nationsencyclopedia.com/...-INFRASTRUCTURE-POWER-AND-COMMUNICATIONS.html
 
Kwanini watu wa JF tusijitolee kulipia Dedicated Server ya Ikulu kama mchango wetu?

Kwani unadhani kuwa Ikulu hawa pesa za kulipia hiyo server? Mbona yule jamaa aliyetengeza website ya maoni alilipwa zaidi dola laki tatu? Si unajua kuwa gharama ya kulipia dedicated server kwa mwaka mzima hazidi hata dola elfu tatu? Ikulu wana hela hizo wala hawahitaji mchango wetu, ila ni washamba tu wa IT.
 



Duh...hivi huko Ikulu kuna watu wamesoma IT kweli??

Mbona tunatia aibu namna hii.?

Wapo tena wana hadi madegree matatu na mishahara kibao wanalipwa.

Hiyo ndiyo Danganyika nchi tuipendayo!

Wembe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…