SoC01 Mmomonyoko wa Maadili katika Jamii: Nini kifanyike kunusuru?

SoC01 Mmomonyoko wa Maadili katika Jamii: Nini kifanyike kunusuru?

Stories of Change - 2021 Competition

mazagazagatza

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2021
Posts
208
Reaction score
224
Maadili ni seti ya mambo ambayo yanamwelekeza mwanajamii atende katika namna ambayo inamjenga yeye na jamii kwa ujumla bila kusababisha migongano.Maadili yanayofaa kwenye jamii kimsingi hufanana kutoka jamii moja kwenda nyingine lakini mazingira yanaweza kusababisha yatekelezwe kwa namna tofauti kiasi.

Pamoja na hayo,binadamu tangu zamani wametoa miongozo maalumu ya maadili kulingana na dini,utamaduni,falsafa nk.

MMOMONYOKO WA MAADILI ni hali ya kukiukwa maadili ya jamii fulani.

Kwa miongo kadhaa,mmomonyoko wa Maadili umesambaa kwa kasi sana hasa miongoni mwa vijana kuliko kwa wazee kutokana na sababu mbalimbali hususani utandawazi,teknolojia,wazazi kutowajibika,makundi rika,uhamiaji katika makazi ya pamoja na mijini,na ndoa mchanganyiko.

Hata hivyo chanzo kikubwa cha mmomonyoko wa maadili ni wazazi na jamii kwa ujumla kutowajibika kikamilifu katika malezi ya watoto na vijana.

MALEZI ni kazi maalumu ambayo binadamu anamsaidia mwingine kukabili maisha kwa ujumla au sehemu yake mojawapo.Malezi ni jukumu la kwanza la wazazi,ambapo nao wanahitaji usaidizi kutoka kwa ukoo,kabila,jamii,dini na taifa kwa ujumla. Ni kazi inayohitaji moyo na ustahimilivu mkubwa!

Siku hizi,watu wengi wameona umuhimu wa kupata elimu ili kufanikiwa katika maisha.Hata hivyo,mara nyingi juhudi hizi hazilengi kuujua UKWELI,bali kufanikiwa katika maisha na uchumi.Na kwa bahati mbaya,zinaweka pembeni maadili yaliyokuwa sehemu muhimu katika malezi ya kimila.

Bila malezi sahihi kwa vijana,kwa kuwa ujana ni kipindi cha mabadiliko ya haraka katika mfumo mzima wa maisha,ni vigumu kuumudu sawasawa na kuwa ma msimamo.

Kutokana na mchanganyiko wa watu;makabila,dini nk.,pamoja na njia mbaya za malezi zinazotokana na mmomonyoko wa maadili,hali ya malezi ni mbaya zaidi mijini.

Siku hizi hata dini ya ukoo siyo kinga tena,kijana anajichagulia mwenyewe aamini nini na aishi vipi badala ya kufuata mazoea ya nyumbani kama alivyofanya utotoni

Kutokana na mabadiliko makubwa kwenye nyanja za elimu,afya,uchumi,mawasiliano,tunu za maisha nk,umbali(gap) kati ya vijana na wazee umekuwa mkubwa mno! Ni kama vile wanaishi Dunia tofauti! Vijana wanaona maisha ya asili ni mambo ya kizamani(kishamba). Wanadharau utamaduni wa mababu kana kwamba mambo yote ya zamani yamepitwa na wakati. Kwa sababu hiyo,wanapokea kwa urahisi mkubwa bila kuhoji mawazo mengi ya kigeni na mitindo mipya inayozuka mijini kupitia vyombo vya habari na vyanzo vingine.

Vijana wanatumia muda wao mwingi kukaa vjiweni na kwenye shughuli za burudani na kukosa muda wa kutosha wa kukaa na wazazi na wazee. Hilo ni pengo lisilozibika kwa kuwa wanapoteza fursa muhimu ya kupata uzoefu halisi na muhimu wa maisha kutoka kwa watangulizi wao.Wanakuwa jamii tofauti,wageni kati ya watu wao! Kwa kweli,maisha ya vijana wa leo yamekuwa tofauti mno na vijana wa zamani.

Ili kukabiliana na changamoto hizi na kunusuru jamii dhidi ya kumomonyoka kwa maadili,wazazi na jamii kwa ujumla bado wanao wajibu wa kuchukua jukumu la kuwalea watoto na vijana katika njia ambazo zitawezesha taifa kupata vijana wanaohitajika,wenye sifa za maadili yanayofaa na ujuzi wa maisha unaotakiwa ili wafanikiwe wao binafsi na jamii kwa ujumla.

Ili kijana azidi kukomaa kiutu anahitaji kusaidiwa na wazazi na jamii ajitambue na kujifahamu ili aweze kustawisha vipawa vyake na kupunguza kasoro zake.

UTU ndio msingi ambao juu yake yanajengwa maisha yote.

Kwa muktadha huu,kama jamii hatuwezi kukubali gharama za mmomonyoko wa maadili na kukaa kimyaa huku tukiangalia taifa letu likizama! Tunatakiwa kusimama kidete kuhakikisha kuwa kila kundi linatimiza wajibu wake kwa kurejea katika njia sahihi za malezi ya watoto na vijana. Tutengeneze mfumo wa kuwatambua watoto na vijana wanaofanya vizuri katika maadili na kuwatuza ili kuwahamasisha kufanya vizuri zaidi na kuwa mifano(model) bora kwa watoto na vijana wenzao. Halikadhalika,tuwapigie kelele wale wote wanaoharibu maadili yetu.Tuwakemee wote wanaoharibu maadili yetu.Katu tusikae kimyaa!
 
Upvote 4
Wanajamvi vipi?
Mbona mnachungulia tu na kupitia?

Naomba mchangie hoja hii tupate namna ya Kunusuru taifa letu dhidi ya mmomonyoko wa maadili.
 
Asante Sana kwa kutukumbusha hili. Kwa kweli tunakoelekea Kama hatutachukua hatua kukabiliana na hili ni hatari Sana.
 
Asante Sana kwa kutukumbusha hili. Kwa kweli tunakoelekea Kama hatutachukua hatua kukabiliana na hili ni hatari Sana.
Mkuu,mmomonyoko wa maadili ni janga la kitaifa kabisa! Tusipochukua hatua,tutakuja kujuta.
 
Kama taifa tunao wajibu wa kutunga sera mahsusi za kulinda maadili yetu. Tunayo haki ya kupinga external influence kwenye masuala yanayolenga kuzorotesha na hata kubadili kabisa mfumo sahihi wa maadili yetu kwa KIGEZO Cha utetezi wa haki za binadamu. Asante kwa mada inayotukumbusha umuhimu wa kulinda maadili yetu
 
Kama taifa tunao wajibu wa kutunga sera mahsusi za kulinda maadili yetu. Tunayo haki ya kupinga external influence kwenye masuala yanayolenga kuzorotesha na hata kubadili kabisa mfumo sahihi wa maadili yetu kwa KIGEZO Cha utetezi wa haki za binadamu. Asante kwa mada inayotukumbusha umuhimu wa kulinda maadili yetu
Mkuu Mogambi asante kwa mchango wako mzuri.

Kutokana na hali kuwa mbaya kabisa kwa upande wa maadili,pengine ni wakati muafaka sasa wakuanzisha harakati za kulinda maadili yetu.

Hasara inayotokana na mmomonyoko wa maadili ni kubwa mno katika jamii!
 
Back
Top Bottom