Mnaacha kutumia Busara kwa kupata Suluhisho la Kudumu ili kuwe na 'Win Win Situation', nyie mnatumia Vitisho mkidhani ndiyo Suluhisho Kuu

Mnaacha kutumia Busara kwa kupata Suluhisho la Kudumu ili kuwe na 'Win Win Situation', nyie mnatumia Vitisho mkidhani ndiyo Suluhisho Kuu

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Jeshi la Polisi Nchini limesema linawatafuta watu waliokula njama kuandaa na kusambaza kwenye mitandao ya kijamii tangazo linalowataka Wafanyabiashara wote wa viunga vya Kariakoo kufunga biashara zao kuanzia Jumatatu ya Juni 24, 2024, bila ukomo, hadi pale changamoto zao za kibiashara zitakapoweza kutatuliwa.

Msemaji wa Jeshi la Polisi Nchini Naibu Kamishna wa Polisi DCP David Misime, ameeleza haya Jijini Arusha ambapo amewahakikishia wafanyabiashara na wananchi wote ambao wanafanya shughuli zao za biashara na kupata mahitaji katika soko la Kariakoo kuwa ulinzi utaimarishwa ipasavyo katika maeneo yote.

Hata hivyo Jeshi la Polisi limetoa wito kwa mtu yeyote mwenye changamoto zenye kuhitaji utatuzi afuate utaratibu wa kuzifikisha kwenye mamlaka husika ili zifanyiwe kazi na sio kuvunja sheria kwa kutoa vitisho na kulazimisha wengine kutekeleza/ kufanya yale ambayo hawakubaliani na waliotoa tangazo hilo.

Aidha DCP Misime amesema kuwa Mbali na tangazo hilo kutokujulikana limetolewa na nani, amebainisha kuwa limeenda mbali zaidi hadi kukiuka sheria za nchi kwa kutangaza vitisho kuwa "Wafanyabiashara watakaokaidi agizo ambalo lilisema kuwa mshale wa jicho utakuwa haki yake".

Chanzo: itvtz

Halafu GENTAMYCINE Kutwa akiwaambia hamna Akili mnakasirika na kununa huku mkimkalia Vikao mumjue ni nani.
 
Screenshot_2024-06-24-15-50-19-1.png
 
Hawa wanyonyaji sana kodi zimekuwa kubwa mnooo maisha yanakuwa ghali wanaendekeza kununua V8 na kujipa maposho makubwa makubwa
 
Back
Top Bottom