mnajua mhamo wa ruwazo? sababu kuu ambayo imeangusha watahiniwa wengi CSEE2012

Mwl Ngasa

Member
Joined
Aug 9, 2012
Posts
32
Reaction score
7
kunasababu nyingi ambazo zmechangia kwa wanafunzi kufeli mtihani kidato cha nne mwaka 2012/2013 lakini mimi kama mwalimu ambae ni mtaalam katika fani hii navyojua kuwa kuna kitu kinaitwa mhamo wa ruwazo "Paradigm shift" yaani kunamabadiliko kidogo juu ya kujifunza na namna ya kupima kama somo limeeleweka kwa anaejifunza "competance based learning" inayoendana na "competance based assesment" sasa zamani tulikua tunajali sana mwanafunzi akumbuke hata kwa kukariri hata na walimu wengi wa sasa walisoma kwa mtindo huo, kwa sasa tunajali sana mwanfunzi awe na maarifa sijui niseme 'ujuzi' yaani hakuna haja ya kukariri ila aelewe! aelewe na akiulizwa maswali ajibu kama mtu anaeelewa sio kukariri, so hapo ndo uwezo wa kujieleza unavyomezwa na lugha kama cmzuri kwenye lugha hapo lazma akwame! na pia walimu wengi bado wanafundisha kwa mtindo wa kizamani! so nivigum sana kumfanya mwanafunzi ajitawale kwa kile atakachofundishwa! ningum kidogo yaani construction of test items and expected answer, technical terms used during assesment na vitu vingi vdogovdogo! Cjui kama nimeeleweka!
 
Ni miongoni mwa sababu. Wanafunzi huwa wanafundishwa kwa tamaduni za kizamani, ili hali wanapimwa kisasa (constructism assessment).
Walimu hawawezi kufundisha 'kisasa' kwa kuwa hawajapewa mafunzo. Mwalimu mmoja anapelekwa mafunzo ya masaa kadhaa (bila ya hata kuelewa au kuuliza maswali), kisha anapewa mamlaka ya kuja kuwafunza waalimu wenzie, waalimu wamekata tamaa, mazingira duni n.k.
Wanafunzi hawawezi kujisomea wenyewe kwa kuwa hawana zana, mazingira duni, jamii haina mwamko, watoto hawajitambui, mmomonyoko mkubwa wa maadili n.k.
Naona nuru inakuja.
 
Nimeangalaia ile PDF ya mkoa wa Arusha na anecdotes za usahihishaji / matatizo ya wanafunzi.

Inabidi tuangalie tena habari ya kufundisha sekondari kwa Kiingereza, ni tatizo kubwa.

Inaonekana kuna watu wengi tu, hasa vijijini huko, ambao hata Kiswahili tabu.

Hawaoni tofauti kati ya kilatini na Kiingereza!

Worse still hao NECTA wenyewe Kiingereza wameboronga, na hawaja proofread muongozo wao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…