Mnakumbuka lakini?

Makaveli_14

New Member
Joined
Sep 1, 2022
Posts
1
Reaction score
0
MNAYAKUMBUKA LAKINI YALE MATUSI YENU??

Walikuwa hawazijuhi shida za kwenye duara kama hawajakutana na huyu mwanaume pale kati.

Wanamkubuka vizuri tu, chini alikuwa anasimama yeye na Victor wa Nairobi halafu mbele yao yupo fundi mmoja kutoka Scandinavia ambaye sasa hivi anawafanya United wasahau kama waliwahi kuwa na Pogba.

Shida ilikuwa inaanzia pale mpira unapotua kwenye miguu yake ila balaa linakuja akiupeleka ule mpira kwenye miguu ya yule fundi wa Scandinavia.

Wakati Christian Eriksen pale Spurs akiufanya mpira uonekane ni kitu ambacho kila mtu anaweza kufanya, nyuma yake alikuwepo huyu mwanaume.

Najua mnakumbuka namna mlivyokuwa mnawatukana mamido wenu wakikutana na show za hiki kiumbe.

Mlikuwa mnawaone bure mamido wenu, akiwa na mpira walijua kabisa anataka kufanya nini, anataka kuupiga pale au kufanya hivi lakini hawakujua njia ya kuuchukua ule mpira kirahisi kutoka kwenye miguu yake.

Waliishia kuuona mpira ukitii maagizo kama anavyotaka yeye na hawakuwa na chaguo lingine zaidi ya kupitia wakati mgumu mbele yake.

Usiku mmoja kwenye dimba la Allianz kule Turin, alikuwa anatoa somo la kukaba na kuachia moja akitumia kitabu cha zamani cha Patrick Vieira wa Arsenal, lile somo lilieleweka vizuri kwa kina Pjanic.hawawezi kulisahau kirahisi lile somo.

Kwanza zilikuwa zinapigwa show za kibabe na mtu mbabe, tabasamu lake ni nadra sana kuliona mkiwa pale kwenye dimba.

Utaona tu kiganja kikubwa cha mkono wake kimekupiga usoni halafu anapita katikati yenu na anaondoka zake.

Kisirisiri mtafute yule Sergio Ramos halafu muoneshe hiyo picha hapo juu, kisha usiendelee kuongea.Sio jina lake tu, atakutajia mpaka mwaka aliozaliwa huyo mwanaume hapo juu.Anamjua vizuri sana

Anaitwa Moussa Dembele, sijui ni kiungo gani sahivi anafanana uchezaji na huyo mbelgiji.Mlikuwa mnashusha matusi mazito kwa viungo wenu.
 

Attachments

  • images (10).jpeg
    18.6 KB · Views: 3
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…