Mnakumbuka niliposhauri John Bocco awe golikipa pale Simba?

SAYVILLE

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2010
Posts
7,895
Reaction score
12,975
Kuna siku nadhani msimu uliopita wakati Simba inapitia changamoto ya nafasi ya golikipa, niliwahi kushauri John Bocco apewe tizi ili awe golikipa. Niliamini angeweza kuwa kipa mzuri kuliko hata Ally Salim.

Kuna watu wakadhani natania au namkosea heshima Bocco.

Kutokana na uzoefu wangu wa kucheza mpira kwa kiwango cha juu sana pamoja na kwamba sikufika level za mapro, kuna kitu kimoja niligundua na nakiamini.

Beki ana nafasi kubwa ya kuwa mshambuliaji mzuri na kinyume chake pia ni kweli. Vivyo hivyo, golikipa ana uwezo wa kuwa mshambuliaji tena mzuri tu hasa striker na kinyume chake pia ni kweli.

Naamini hivyo kwa sababu mfano kwa beki umecheza miaka mingi ukikabiliana na washambuliaji, inafika wakati unajua jinsi wanavyofikiri.

Siku ukiambiwa ubadili nafasi inakuwa rahisi kucheza nafasi yake maana akili tayari inaweza kufikiri kama mtu huyo.

Tena unakuwa na advantage ya ziada, unakuwa na uwezo wa kufikiri kama beki pia kwa hiyo unakuwa na uwezo wa ziada wa kuwashinda mabeki.

Muogope sana mchezaji aliyeswitch nafasi kama hizo, yaani ameanza kama beki akahamia mshambuliaji au kinyume chake, au kipa akahamia kuwa mshambuliaji, au kinyume chake. Huwa wanakuwa wazuri sana.

Mifano ya haya kutokea ipo tena mingine hapa hapa Tanzania.

Kuna golikipa wa TP Mazembe, Suleiman Shaibu ameprove theory yangu kuwa ni kweli maana sasa hivi kageuzwa striker na anatupia magoli sio poa.

Soma hii mada ya Bocco: John Bocco aandaliwe kama golikipa wa akiba
 
Kuna siku nadhani msimu uliopita wakati Simba inapitia changamoto ya nafasi ya golikipa, niliwahi kushauri John Bocco apewe tizi ili awe golikipa. Niliamini angeweza kuwa kipa mzuri kuliko hata Ally Salim. Kuna watu wakadhani natania au namkosea heshima Bocco.

Kutokana na uzoefu wangu wa kucheza mpira kwa kiwango cha juu sana pamoja na kwamba sikufika level za mapro, kuna kitu kimoja niligundua na nakiamini. Beki ana nafasi kubwa ya kuwa mshambuliaji mzuri na kinyume chake pia ni kweli. Vivyo hivyo, golikipa ana uwezo wa kuwa mshambuliaji tena mzuri tu hasa striker na kinyume chake pia ni kweli.

Naamini hivyo kwa sababu mfano kwa beki umecheza miaka mingi ukikabiliana na washambuliaji, inafika wakati unajua jinsi wanavyofikiri. Siku ukiambiwa ubadili nafasi inakuwa rahisi kucheza nafasi yake maana akili tayari inaweza kufikiri kama mtu huyo. Tena unakuwa na advantage ya ziada, unakuwa na uwezo wa kufikiri kama beki pia kwa hiyo unakuwa na uwezo wa ziada wa kuwashinda mabeki.

Muogope sana mchezaji aliyeswitch nafasi kama hizo, yaani ameanza kama beki akahamia mshambuliaji au kinyume chake, au kipa akahamia kuwa mshambuliaji, au kinyume chake. Huwa wanakuwa wazuri sana.

Mifano ya haya kutokea ipo tena mingine hapa hapa Tanzania.

Kuna golikipa wa TP Mazembe, Suleiman Shaibu ameprove theory yangu kuwa ni kweli maana sasa hivi kageuzwa striker na anatupia magoli sio poa.

Soma hii mada ya Bocco: John Bocco aandaliwe kama golikipa wa akiba
Simba hawakupitia magumu kiasi hicho. TP Mazembe hawana uwezo wa kusajili mchezaji yeyote inawalazimu kumuongeza kipa wao wa akiba kama mshambuliaji. Vinginevyo hayo yasingekuwepo. Japokuwa sikatai mchezaji anaweza badilishwa position na akawa mzuri; mfano Djigui Diarra aliitwa timu ya vijana Mali(U17) kama attacking midfielder akabadilishwa kuwa kipa, Clement Mzize amekua akicheza ndondo beki na kiungo mkabaji alipoingia timu ya vijana Yanga akaanza kama striker. Huyu naamini atamaliza mpira wake akiwa beki😀😀😀. Pia Said Nassoro Mwamba "Kizota"(R.I.P) amekuwa star mkubwa Afrika Mashariki na Kati kama striker na awards kibao ila Mashindano ya CECAFA(Kagame) ya 1999 Kampala alishushwa kucheza beki namba 5 baada ya Ally Mayai Tembele kula umeme mapema first half. Baada ya hapo tukasahau kama Kizota ni forward mkali. Na ubingwa Yanga tukaubeba kibabe sana. Hadi anastaafu ni beki mwamba haswaa...dizaini ya Bacca😀😀😀. Simba wangepitia wanayopita TP Mazembe labda tungemuona Bocco kwny milingoti. Ndo vionjo vya soka letu hivyo😀😀😀
💪
 
Umejikita sana kuangalia sababu ya nini kimesababisha mchezaji kubadili nafasi badala ya kuangalia msingi wa hoja ambao ni mchezaji kubadili nafasi, kama kwenda kinyume cha nafasi yake ya awali na kuwa bora.
 
At a pro level, hizo cases ni chache sana mkuu. Kwa uelewa wangu mostly lazima kuwe na sababu lazimishi kumtoa mtu kutoka eneo moja kumpeleka lingine kwa kipa, beki na striker. Unless iwe kwa level za chini(U17,U18, n.k). Ukishafika level za juu kama hiyo ya Bocco unayosema siyo maamuzi rahisi hivyo kwa kukariri tu kuwa "huwa wanakuwa wazuri". No one is ready to take that risk, iwe mchezaji mwenyewe, management yake, benchi la ufundi, klabu husika na hata mashabiki pia. It takes a lot kumpata John Bocco the same to Aishi Manula au Ibra Bacca. Huwezi kirahisi tu kuswitch from Bocco to Manula au Bacca to Bocco....Ilazimike kuwa hivyo, sawa ila siyo jambo la kulifikiria kirahisi rahisi.
 
Mimi mwenyewe enzi zangu nilikuwa beki mkatili sana! Ila siku nilipojaribishwa kucheza namba 9!

Aisee mpaka leo nina mvi za kutosha tu kichwani, lakini bado natupia magoli kwenye mechi za maveterani. Na huenda nikawa veterani mzee kuliko wote nchini.
Utoto raha sana. Yaani dogo uko hapo unanyonya kidole tayari unajiwazia kuwa wewe mzee
 
At a pro level, hizo cases ni chache sana mkuu. Kwa uelewa wangu mostly lazima kuwe na sababu lazimishi kumtoa mtu kutoka eneo moja kumpeleka lingine kwa kipa, beki na striker. Unless iwe kwa level za chini(U17,U18, n.k). Ukishafika level za juu kama hiyo ya Bocco unayosema siyo maamuzi rahisi hivyo kwa kukariri tu kuwa "huwa wanakuwa wazuri". No one is ready to take that risk, iwe mchezaji mwenyewe, management yake, benchi la ufundi, klabu husika na hata mashabiki pia. It takes a lot kumpata John Bocco the same to Aishi Manula au Ibra Bacca. Huwezi kirahisi tu kuswitch from Bocco to Manula au Bacca to Bocco....Ilazimike kuwa hivyo, sawa ila siyo jambo la kulifikiria kirahisi rahisi.
Sidhani kama nimesema ni jambo rahisi. Naelewa kuwa asilimia kubwa ya matukio hayo yanafanyika pale umuhimu wa kufanya hivyo unapohitajika ila kama nilivyokwishasema, siyo msingi wa hoja yangu! Sielewi kwa nini unashindwa kuelewa hilo.

Manula alipoumia, mabeki wa Simba walikuwa wanashindwa hata kurudisha mpira kwa kipa wakijua Ally Salim hana footwork nzuri. Tahadhari iliongezeka, pamoja na kwamba kucheza kwa tahadhari ni jambo jema ila iliharibu flow ya timu.
 
Sasa Bocco ndo angesolve tatizo? Utayari wake ulikuwaje?
 
Simba hawakupitia magumu kiasi hicho. TP Mazembe hawana uwezo wa kusajili mchezaji yeyote inawalazimu kumuongeza kipa wao wa akiba kama mshambuliaji. Vinginevyo hayo yasingekuwepo. Japokuwa sikatai mchezaji anaweza badilishwa position na akawa mzuri; mfano Djigui Diarra aliitwa timu ya vijana Mali(U17) kama attacking midfielder akabadilishwa kuwa kipa, Clement Mzize amekua akicheza ndondo beki na kiungo mkabaji alipoingia timu ya vijana Yanga akaanza kama striker. Huyu naamini atamaliza mpira wake akiwa beki😀😀😀. Pia Said Nassoro Mwamba "Kizota"(R.I.P) amekuwa star mkubwa Afrika Mashariki na Kati kama striker na awards kibao ila Mashindano ya CECAFA(Kagame) ya 1999 Kampala alishushwa kucheza beki namba 5 baada ya Ally Mayai Tembele kula umeme mapema first half. Baada ya hapo tukasahau kama Kizota ni forward mkali. Na ubingwa Yanga tukaubeba kibabe sana. Hadi anastaafu ni beki mwamba haswaa...dizaini ya Bacca😀😀😀. Simba wangepitia wanayopita TP Mazembe labda tungemuona Bocco kwny milingoti. Ndo vionjo vya soka letu hivyo😀😀😀
💪
Asante kwa historia fupi na nzuri ya Mwamba Kizota legend
 
At a pro level, hizo cases ni chache sana mkuu. Kwa uelewa wangu mostly lazima kuwe na sababu lazimishi kumtoa mtu kutoka eneo moja kumpeleka lingine kwa kipa, beki na striker. Unless iwe kwa level za chini(U17,U18, n.k). Ukishafika level za juu kama hiyo ya Bocco unayosema siyo maamuzi rahisi hivyo kwa kukariri tu kuwa "huwa wanakuwa wazuri". No one is ready to take that risk, iwe mchezaji mwenyewe, management yake, benchi la ufundi, klabu husika na hata mashabiki pia. It takes a lot kumpata John Bocco the same to Aishi Manula au Ibra Bacca. Huwezi kirahisi tu kuswitch from Bocco to Manula au Bacca to Bocco....Ilazimike kuwa hivyo, sawa ila siyo jambo la kulifikiria kirahisi rahisi.
We Jamaa unajua mpira.
 
Kuna siku nadhani msimu uliopita wakati Simba inapitia changamoto ya nafasi ya golikipa, niliwahi kushauri John Bocco apewe tizi ili awe golikipa. Niliamini angeweza kuwa kipa mzuri kuliko hata Ally Salim.

Kuna watu wakadhani natania au namkosea heshima Bocco.

Kutokana na uzoefu wangu wa kucheza mpira kwa kiwango cha juu sana pamoja na kwamba sikufika level za mapro, kuna kitu kimoja niligundua na nakiamini.

Beki ana nafasi kubwa ya kuwa mshambuliaji mzuri na kinyume chake pia ni kweli. Vivyo hivyo, golikipa ana uwezo wa kuwa mshambuliaji tena mzuri tu hasa striker na kinyume chake pia ni kweli.

Naamini hivyo kwa sababu mfano kwa beki umecheza miaka mingi ukikabiliana na washambuliaji, inafika wakati unajua jinsi wanavyofikiri.

Siku ukiambiwa ubadili nafasi inakuwa rahisi kucheza nafasi yake maana akili tayari inaweza kufikiri kama mtu huyo.

Tena unakuwa na advantage ya ziada, unakuwa na uwezo wa kufikiri kama beki pia kwa hiyo unakuwa na uwezo wa ziada wa kuwashinda mabeki.

Muogope sana mchezaji aliyeswitch nafasi kama hizo, yaani ameanza kama beki akahamia mshambuliaji au kinyume chake, au kipa akahamia kuwa mshambuliaji, au kinyume chake. Huwa wanakuwa wazuri sana.

Mifano ya haya kutokea ipo tena mingine hapa hapa Tanzania.

Kuna golikipa wa TP Mazembe, Suleiman Shaibu ameprove theory yangu kuwa ni kweli maana sasa hivi kageuzwa striker na anatupia magoli sio poa.

Soma hii mada ya Bocco: John Bocco aandaliwe kama golikipa wa akiba
Toa mifano.
 
Huyo kipa wa TP Mazembe ametupia ngapi mpaka sasa?
 
Asante kwa historia fupi na nzuri ya Mwamba Kizota legend
Mwamba ana historia kubwa kuliko nilichokisema hapo. Watu wanasimulia mabalaa yake tangu akiwa Dodoma (Kurugenzi au Waziri Mkuu kama niko sahihi....timu za miaka hiyo😀😀😀) na alipotua tu Jangwani akabatizwa jina la Kizota. Sisi wa mikoani tulikuwa tunafuatilia redioni tu so kama tulidanyanywa ndo basi tena. Ila jamaa alikuwa anatupia magoli haswaa. Kwa msimu mmoja unaweza bahatisha kuiona Yanga mara moja tu kama mkoa wako kuna timu ya daraja la kwanza/Ligi kuu. Stories nyingi ni magazetini na redioni tu. Tumeanza kuwaona miaka ya 90 mwishoni ITV walipoanza kurusha baadhi ya michuano kama CECAFA na CAF. Hatuwafaidi sana kama tunavyowaona hawa akina Nkane zama hizi.😀😀😀
 
Back
Top Bottom