Paspii0
JF-Expert Member
- Apr 10, 2020
- 346
- 522
👉🏾Enyi kizazi cha 2000! ,nafuraha kukujuza yafuatayo!
Kadiri ya mapokeo ya Kanisa, tarehe 14 Februari inahusishwa na kumbukumbu ya Valentine, ambaye alikuwa kasisi aliyeishi katika karne ya tatu.
Hadithi ya kasisi Valentine inasema kwamba alikamatwa na kuuliwa kwa sababu ya kuendelea kufundisha imani ya Kikristo na kuwaasa vijana kuingia kwenye ndoa na kuishi vyema bila kuendelea na dhambi ya uzinifu na uasherati, ikumbukwe wakati wa utawala wa Mfalme Claudius II, ambaye alikataza ndoa kwa vijana akiamini kuwa bila kuwa na familia, wanajeshi wangeweza kuwa bora vitani.
Valentine alikiuka agizo hili kwa kuunganishia wanandoa wapya na alikuwa akijulikana kwa wema wake na huduma kwa waliokuwa katika shida.
Katika mapokeo ya Kanisa, tarehe 14 Februari ni siku ya kukumbuka upendo wa kweli, huruma, na kujitolea kwa ajili ya wengine, na siyo tu kusherehekea mapenzi ya kimwili. Tunapaswa kuzingatia upendo wa Mungu na jinsi upendo wa Kimungu unavyohusiana na uhusiano wa kibinadamu.
👉🏾 Nyie watoto wa 2000 tuelewane hapa ,Wengi hamna ufahamu wa hadithi kamili ya siku ya Valentine na sababu halisi ya kumbukumbu hii. Hivyo mmesababisha baadhi ya watu kusherehekea tarehe hii bila kujua maadili ya msingi ya Kikristo, ambayo ni upendo wa kujitolea, heshima, na kujali wengine bila kujali hali yao,Ajabu wazinzi ndio wanaiadhimisha siku hii kwa uchu kuliko uhalisia wa kuikataa dhambi!! Ajabu mtafyeka viwanja na makwanja kama nini 😤😤
👉🏾Nyie watoto wa 2000, nawaambia hivi Wekeni kando matarajio ya kipekee kuhusu siku hii na kuhusu zawadi za kifahari na sherehe kubwa. Tafakarini juu ya maana halisi ya upendo na jinsi unavyoweza kuonesha upendo kwa njia rahisi lakini yenye maana. Huenda zawadi ndogo kama ujumbe wa shukrani au msaada kwa wale wanaohitaji ikawa na maana kubwa zaidi kuliko vitu vya kifahari na vizawadi vya mchongo 😊😊 mnaliwa kizembe sana nyie watoto wa 2000.
Haya herini kwa kumbukizi za Mt.Valentino ! ,ujumbe fungeni ndoa ,ishini katika hali safi ,tutajenga taifa bora lenye hofu na kiu ya kumjua Mungu.