Mnamtaka Okwi? Timizeni haya masharti.

Mnamtaka Okwi? Timizeni haya masharti.

lil wayne

JF-Expert Member
Joined
Apr 15, 2016
Posts
992
Reaction score
904
Mshambuliaji nyota wa zamani wa Simba , Emmanuel Okwi, yuko tayari kuondoka Denmark na kujiunga nao tena lakini fedha, ndiyo tatizo kubwa . Okwi amesema yuko tayari kuondoka klabu ya Sonderjyske inayoshiriki Ligi Kuu Denmark ili arejee Simba , lakini yeye na klabu hiyo zimetoa masharti kwa Simba.

1. Sharti la kwanza ambalo wamelipata Simba kutoka kwa klabu hiyo ya Sweden ni kurudishiwa kitita cha dola 120,000 (zaidi ya Sh milioni 250 za Kibongo au wengine huziita pesa za madafu) ambazo walimnunua Okwi kutoka Simba kipindi kilichopita.

2. Sharti la pili ambalo wamepewa Simba ni kutoka kwa Okwi ambaye amesema kweli yuko tayari kurejea, lakini mshahara apewe dola 5,000 (zaidi ya Sh milioni 12 yaani kwa [HASHTAG]#MWEZI[/HASHTAG]).

Haya kazi kwenu sasa wenye ndoto za kumleta Okwi. ila nasikia ubingwa mpaka utimize miaka 6 bila ndoo, ndipo utakuja beba tena.

Washaulini viongozi wenu, Kama mna malengo ya dhati ya kumnunua Okwi ni bora mzilete kwetu(Yanga SC) hizo mil250 ili tuwauzie kati ya Deus "Götze" Kaseke au Juma "Podolski" Mahadhi....ila siyo huyo Okwi maana misimu yake 2 ya mwisho kuwa na simba hakuwasaidia chochote, alishuhudia ndoo zikienda Yanga SC na Azam FC tu.
 
Back
Top Bottom