Mnao kwamisha mageuzi Yanga Sc mnakera

ntamaholo

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2011
Posts
12,938
Reaction score
6,942
Wana bodi

Moja ya sababu kwa nini Tanzania hatufanyi vizuri kimataifa, ni kukosa uwekezaji makini kwenye vilabu vyetu halafu kutegemea kuhonga na uchawi kuendesha masuala ya mpira.

Niwapongeze Simba Sc kukubali mabadiliko na kuamua kukabidhi timu, na hii imewasaidia, maana kwa sasa mashabiki wa simba kwa timu za ndani, wanaingia kwa wingi maana ushindi kwao ni lazima, siyo bahati.

Nakumbuka Yanga iliitisha mkutano mkuu kwa ajili ya kurekebisha katiba, lkn mkutano huo umeshindikana baada ya watu kupeleka kesi mahakamani.

Naamini wanaozuia mchakato huo ni aidha ni mashabik wa simba hivyo wanapambana kuhakikisha Yanga haimpi simba upinzani au wanawaza matumbo yao jambo ambalo limepelekea mashabiki wa Yanga kuyokuwa na confidence juu ya timu yao. Suala hili ni dhahiri, maana hata uingiaji uwanjani, simba wanaingia zaidi huku Yanga tukiogopa.

Mnaozuia mabadiliko ndani ya Yanga, mnakwamisha maendeleo ya timu, na mnakwamisha maendeleo ya taifa kimchezo. Bora mkufe mtuachie timu yetu kwa kweli.

Badilikeni, tuleteeni furaha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Both of them mkuu,simba wenye madaraka yao wanawatumia wajumbe flan wa kamati ya utendaji waliogoma kujiuzulu na tff ili Yanga isipige hatua yoyote,hali inayokumbana nayo Yanga kwa sasa haijaja kwa bahati mbaya,ni mkakati umepangwa na watu wenye mapenzi na simba walioko serikalini
 
Aisee!! Yanga acheni visingizio vya kusingizia serikali. Wakati wa "Yanga Ukuta" na
"Yanga Kampuni" serikali ilikuwa upande upi? Mngemsikiliza Tarimba leo hii mngekuwa mbali sana!!
 
Unataka kusema Bashite anahujumu Yanga?ili apate nini
 
Kuna kiongozi wa zamani wa simba anaitwa shikamkono Alisema kwenye gazeti moja kuwa miaka ya nyuma kuna kiongozi wa simba alikosa uongozi akaenda Yanga. Sasa kiongozi kama huyo ataenda kutetea maslahi ya Yanga?? Hii migogoro inasababishwa Maalumu kuporomosha timu. Kwanini katiba ya Klabu isifuatwe hata kiongozi akihujumu asimamishwe?
 
Ujinga wa kwenda mahakamani mwende wenyewe halafu mtafute visingizio.Ujahili ni udhalili. Pukachaka.
 
Sina Koment mmejitakia wenyewe.
Kati yenu kuna Yanga Asili na Yanga Kampuni.
Kumbukeni ninyi wenyewe mlichagua nini wakati ule.
Wenzenu wamechagua Kampuni na wanasonga.
Nyie Asili hadi mlimpiga mawe yule mzee tajiri.
Na mkashinda nia yenu.
Sasa kelele za nini.
Hata kuchagua Mwenyekiti mnashindwa
Mtaweza kuchagua mabadiliko.
Kifo cha Panzi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hadi waziri mwakembe na rais wa tff wanashiliki kuihujumu yanga

Sent using Jamii Forums mobile app
Huu ujinga ndio unawaangamiza. Yaan mna njaa hadi kila mtu mnamuona adui. Hatua mliyofikia mnahitaji kupata tiba ya kisaikolojia au hospitali ya vichaa! Yaan mna matatizo halafu mnakataa. Kama ni mgonjwa wa ngoma mko denial stage, mnahitaji msaada mkubwa!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Reactions: Tui
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…