Mnaoandika R badala ya L Ni kwamba hamuoni vizuri ama?

Sun is Sun

JF-Expert Member
Joined
Mar 13, 2024
Posts
1,254
Reaction score
2,014
Wale wa chakura, Kurara, kumariza, kura, arisema, arikuwa.

Binafsi nikishaona mtu anaandika hivyo nampunguzia alama.
 
Tatizo unadanganywa Kwa kudhani kila mtu ni msomi humu.

Humu form four failure ni wengi kuliko unavyodhani.

Yaani mtu anaandika hivi

Ujasili
Mazingila
Ukweri
Darari.

Au wapo wanaoandika hivi

Utoi _Hutoi
Halikosea _alikosea

Ayupo_Hayupo
Himetoka_imetoka
 
Tunaona Vizuli tuu

Kitu cha msingi usome na uerewe sii ndio mkuu😁
 
Lugha ya Kiswahili inakufa kwenye uandishi
Herufi “H” haitumiki kwenye maneno mengi
hadi - adi
Hela - ela

Na watu hawa wameweza kupenya mpaka kufika kwenye vyombo vikubwa vya habari hivyo kufanya matumizi ya R na L pamoja na H kuonekana jambo la kawaida pale yasipotumika mahala pake


“Mahali na Mahari ni vitu viwili tofauti kabisa“
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…