Mnaodai Kocha Robertinho amevutiwa na Kibu Dennis mmehongwa

Mwishokambi

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2020
Posts
390
Reaction score
1,425
Eti mitandao yote Leo imeandika kwa pamoja na maneno yale yale kuwa kocha mpya amevutiwa na uwezo wa Kibu na atambadilisha, huo ni uongo mtupu na ni mchongo tu wa kutaka mchezaji huyo ambaye ana mtu ndani ya Simba anampigia chapuo ndio analazimisha abaki

Ukweli Kibu hamfikii hata kidogo Dickson Ambundo, Kibu sio wa kuchezea Simba, kwanza ni mzito, hatumii akili, hajiamini, hana control, huyo mbrazil sio mjinga kiasi mnataka kumgombanisha na mashabiki

Kibu hana tofauti na Karim Mandonga, angekuwa kwenye boxing angefanya vizuri sana, simsemi vby ila kuendelea kumpaisha kimchongo ni upuuzi tu.
 
Kwani kibu Ni mchezaji mmbaya kiivo .?

Class is permanent, form is temporary !
 
Kibu Denis Prosper

Mchezaji anayejituma, mwenye nidhamu, anayehitaji kuwalipa mashabiki angalau thamani yake iendane na klabu anayochezea.

Lakini hana bahati, yes BAHATI ni kitu kikubwa sana kwenye upambanaji.
Ukiwa na bahati unaweza kuikwepa hata risasi iliyofyatuliwa umbali wa mita mbili.

Ukiwa na bahati unaweza kupewa uongozi/utawala , mamlaka ya juu, hata kama ni kichwa maji.
 
Kibu ni mchezaji mwenye potential sana, kuna jambo sehemu limevurugika, sijui ni la kiroho au kisaikolojia lililofunga uwezo wake.

Huo ni mtazamo wangu wa haraka haraka.
 
Nilishangaa Kibu anabaki halafu Kagere anaondoka..amefurahishwa nae kwa lipi maana ile mechi yetu ya Ndoige juzi hamna alichofanya.
 
Nilishangaa Kibu anabaki halafu Kagere anaondoka..amefurahishwa nae kwa lipi maana ile mechi yetu ya Ndoige juzi hamna alichofanya.
Mimi sikushangaa kwa sababu nina uelewa wa kutosha. Ninajua idadi inayoruhusiwa ya wachezaji wazawa ni kubwa kuliko wageni. Nilitegemea utalinganisha mzawa kwa mzawa, mgeni kwa mgeni
 
Mimi sikushangaa kwa sababu nina uelewa wa kutosha. Ninajua idadi inayoruhusiwa ya wachezaji wazawa ni kubwa kuliko wageni. Nilitegemea utalinganisha mzawa kwa mzawa, mgeni kwa mgeni
Ahsante
 
Kibu si mchezaji mbaya kwa kiasi hicho unachotumia nguvu kuwaaminisha wenye macho. Hao makocha wa Taifa Stars kwa nyakati tofauti tofauti walizokuwa wakimuita Kibu, nao walirubuniwa?
 
Kibu ni mchezaji mwenye potential sana, kuna jambo sehemu limevurugika, sijui ni la kiroho au kisaikolojia lililofunga uwezo wake.

Huo ni mtazamo wangu wa haraka haraka.
Anyang'anywe uraia wa Tanzania atacheza kama foreign professional player atajiamini.
Bila hivyo baba mmh.
Huyu Waziri na Ofisa aliyemshauri apewe Uraia wa Tanzania kwa kuupiga mwingi hivyo ataisaidia nchi yetu nao inafaa wasipimwe mkojo tu bali mpaka mavi maana inawezekana kuna mirija au mishipa imeingiliana baina ya chemba ya nnya na ubongo hivyo wakati wa maamuzi huenda viliingiliana.
 
Uraia anapewa mtu yeyote anayeomba na kukidhi vigezo, si lazima awe mchezaji. Hata wewe pamoja na kwamba hauna fani yoyote, unaweza ukaomba uraia wa Burundi na ukapewa
 
Hata guardiola alimpenda sterling.

Iko hivi kocha anaweza kumpenda mchezaji sababu ya vitu fulani na kumchukia sababu ya vitu fulani,

Mfno kocha huenda kaona kibu ana nguvu, na vingine ila anakosa utulivu anaamini kwake anaweza mtuliza akabadilisha na kumfanyia kazi yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…