Mnaohamishia maneno ya Utani ya JF na kuyapeleka mitaani kuweni makini mtaumia!

Mnaohamishia maneno ya Utani ya JF na kuyapeleka mitaani kuweni makini mtaumia!

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Hivi naandika huu Uzi kuna Mtu mmoja sasa nimemsindikiza kumpeleka kupata huduma ya Kwanza baada ya kupata Kipigo cha Shalubela / Hatari kutoka kwa Mtu ambaye alimtania na lile neno ambalo huwa linapenda sana kutumika humu JF na nahisi huyo ' Mhanga ' wa Kipigo hicho atakuwa ni mwana JF tu.

Wamebishania mambo ya Siasa kisha mara ghafla nikasia ' Mpigaji ' anaambiwa asiwe kama Mwanaume wa Dar ndipo nikaona Mtu kapigwa Kichwa ambacho sidhani hata aliyekuwa Mfungaji bora wa magoli ya Vichwa nchini Tanzania Abeid Mziba Tekero alikuwa akivipiga hivi.

Hii ni mara ya pili nashuhudia Mtu anapata Kichapo / Kipigo kutokana na ' matani ' ambayo mara nyingi huwa nayaona humu Jamvini ambapo kuna Siku nilishuhudia tena Mtu akipigwa ' Kibao ' kitakatifu baada ya kumuita mwenzake Popoma ( neno linalomaanisha Pumbavu ) ambapo hadi alizimia na kugundua kwamba yule aliyempiga Kibao lazima tu atakuwa alikuwa ni Mjeda / Mwanamedani.

Nitoe Rai kwenu tafadhalini tutaniane tu humu humu Jamvini na haya maneno yetu lakini chonde chonde msihamishie haya maneno yetu humu na mkayapeleka huko mitaani kwani mtaumia na hasa mkizingatia Watu wengi sasa hivi wana ' stress ' zao za Kimaisha.

Nawasilisha.
 
Mwanaume wa Dar ana tatizo gani kwani......Waliomchukua Roma walikuwa wanaume wa wapi kwani?
 
Juzi kati kuna Chalii nimesikia akimuita mwenzake jiwe arif
 
"Mwanaume wa Dar" limeanza kutumika kabla JF haijaanzishwa
 
Mwanaume wa Dar ana tatizo gani kwani......Waliomchukua Roma walikuwa wanaume wa wapi kwani?

Kumbe unawajua kuwa waliomchukua Roma Mkatoliki walikuwa ni Wanaume wa Dar sasa mbona kama unawajua / uliwajua hujaenda kuwasaidia Police Tanzania ili waweze kuwakamata kusudi tatizo lile lililokuwepo la ' Utekaji ' Watu liweze kumalizwa / kukabiliwa kabisa na liwe historia Tanzania?
 
Roma mwenyewe kashindwa kusema.Muulize kama hawakuwa wa Dar
 
ni udhalilishaji wa kijinsia na fedhea kuitwa mwanaume wa dar hata kama ni mm lazima nikupige
 
Inasikitisha sana...

Ila JF inavyotumiwa aiseee... humu kuna members kibao... ila mtaani huwasikii kabisa wakijinasibu wao ni watumaiji wa JF au hata kuifahamu...

Na hata ukikuta App ya JF kwa mtu, ukimuliza kumbe nawe ni member wa hii forum. Utasikia toka ni-install sijawahi hata kuitumia...

Cc: mahondaw
 
Back
Top Bottom