Mnaoishi na chawa mmegundua siri gani?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2023
Posts
7,189
Reaction score
10,375
Kule kwetu watu wenye chawa walikuwa wakijisikia aibu, lakini nasikia huko kwenu ni ufahari kuwa na chawa wengi!

Kule kwetu tulikuwa tukuzichemshia maji nguo zenye chawa, lakini nasikia huko kwenu mnazilisha na kuzihudumia vizuri!

Kule kwetu tulikuwa tukikosa usingizi chawa wakivamia vitanda vyetu, lakini nasikia huko kwenu wanawafanya mlale usingizi mnono!

Kule kwetu chawa walipatikana kwa watu wachafu, lakini nasikia huko kwenu mnawatengeneza kwa makusudi!

Kikwetu, kuwa na chawa ni uchafu, aibu, na fedheha! Ni tofauti kabisa na ninyi mnaoona fahari kuwa nao!

Ni nini mlichogundua kwa chawa kilichowapelekea kuwapenda?
 
Chawa wa Mama
 
Kuwa chawa ni wezi na waporaji😅
 
Binafsi nina allergy na chawa na ndiyo maana nawawinda kina Mwijaku, Baba Levo, Dotto Magari na Steve Nyerere niwaogeshe maji ya moto au kuwachoma kabisa moto nikiwaona.
 
CCM UJUMBE WENU NA CHAWA WENU
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…