Jibaba Bonge
JF-Expert Member
- May 6, 2008
- 1,246
- 402
Nimesoma posts nyingi sana humu za baadhi ya watu na naona ni wale wanaompinga Dr. Slaa. wengi wao wanasema huyu ni mkatoliki mara ni padre n.k.
napenda kutoa angalizo kwa watu hawa, unapo-propagate udini na kuwafanya watanzania wamchague raisi wao kwa misingi ya dini madhara yake yatakuwa makubwa sana. kwa sasa unaweza kufikiri ni mbinu nzuri ya kumdhoofisha mgombea mmoja dhidi ya yule unayempenda. VITA ya kidini itakapoanza usifikiri wewe utapona - As long as wewe ni mtanzania na unaisha Tanzania utakuwa victim wa vita hiyo na hata kama utakuwa unaishi nje ya tanzania bado utakuwa victim tu hata kama ni indirectly.
Nchi ikiingia kwenye vita ya kidini hutapona na machafuko yake ni vigumu sana kuyazima kwa maana ni suala linalohusu imani za watu.
Hivi unaweza kumpata raisi Tanzania asiye na dini? kama hatakuwa muislam atakuwa mkristo ama mhindu ama mwenye dini ya kipagani! Mnaposema aaa huyu ataongoza kiislam au kikristo / kikatoliki ama kidini yoyote ile, hivi tanzania haina katiba? Akiongoza atakavyo si atakuwa amevunja katiba?
Hebu mpigieni kampeni mtu kwa merits zake za kiuongozi na maadili mema siyo dini yake?
mbona wote waliotajwa kuwa mafisadi wana dini zao? wengine waislam wengine wakristo na wangine wana dini nyingine mbalimbali lakini wote hawakuwa na maadili mema.
Just imagine, kundi moja likiinuka na kusema Dr. Slaa ni mkristo-mkatoliki asichaguliwe na lingine likaja na kusema Kikwete ni muislam ataisilimisha nchi tusimchague kweli tutampata raisi?
Tuachane na mambo ya kidini katika kumchagua raisi. Jengeni hoja zenye nguvu katika kumnadi mnayempenda siyo kutuletea machafuko nchini mwetu.