Bila bila
JF-Expert Member
- Dec 20, 2016
- 22,168
- 39,118
Jana kulikuwa na Mechi iliyobayizwa jina la Derby ya Dar es salaam Kati ya Yanga na Azam iliyomalizika Kwa matokeo ya 2-2. Kama ilivyo kawaida ya Mechi ngumu haikosi matukio. Kinachotrend Kwa Sasa zaidi ya matokeo ni maamuzi ya mwamuzi wa Mechi ya Jana katika baadhi ya matukio aliyopaswa kuamua vinginevyo.
Kwa Leo hiyo si hoja yangu. Hoja yangu ni jinsi wanaoitwa wachambuzi wa soka àmbao Kwa nchi nyingine watu wanawategemea kusikia maoni yaliyoshiba wanavyobebwa na ushabiki na kuchambua Kwa uelekeo wa mapenzi Kwa timu.
Nikichukua Mechi 3 zilizozua mijadala zaidi nchini ikiwemo ya Jana nawaona wachambuzi kama wachochezi katika matukio badala ya kukosoa Kwa Nia ya kujenga.
1.Coast Union Vs Yanga tukio la faulo ya Mtenje Jr dhidi ya Bangala halikupaswa kuwagawanya wachambuzi wakawepo wa kulaani tukio na mwamuzi Kwa kutochukua hatua sitahiki na wale wanaotetea tukio lile eti rafu ni sehemu ya mchezo na maamuzi ya refa ni madhaifu ya kibinadamu. Kesho Mtenje atafanya tena Kwa vile alipata watetezi, itamgharimu yeye na timu yake akichukuliwa hatua sitahiki na itamgharimu mchezaji atakayeumizwa na inaweza kuwa mwisho wa maisha yake kisoka tukapoteza kipaji.
2.Yanga Vs Simba Ngao ya hisani limejadiliwa Sana tukio la Inongà dhidi ya Salim Abubakar. Eti nalo lilipata watetezi kwamba Kwa vile Salim alimkwepa na kisha kureact basi refa alitumia busara. Ni kweli hakimu apaswa kuwa na busara, lakini kutoa hukumu ya haki ni busara pia. Hata kama angemtoa na Salim Abubakar bado ingekuwa busara na ingewaonya wote wawili wasirudie waliyoyafanya.
3.Komesha ni Jana Yanga Vs Azam
Wapo na hata Kwa majina wamejiandika wanaoona "busara" ya Refa Kwa kitendo cha rafu mbaya ya Bajana dhidi ya Job iliyopelekea kutoendelea na mchezo ni Jambo zuri. Lakini Huyo Huyo anayeona Bajana ambaye hakuadhibiwa ipasavyo na ikampa kichwa akamfanyia rafu nyingine mbaya Bernard Morrison, ndio wanaoona refa hakutenda busara kutomwonyesha Kadi nyekundu mchezaji aliyefanya Upumbavu na unyama uliopitiliza Bernard Morrison dhidi ya Lusajo Mwaikenda. Hakuna busara njema ya kuacha mhalifu aendelee bila adhabu.
Kitendo cha Bajana na Morrison kumaliza salama Mechi ya Jana kwangu ni doa kubwa Kwa mwamuzi. Huwezi kuwa na Wachezaji wanaofikiria kuumiza wenzao uwanjani wakati wao wakiumizwa wanalalamika. Ningemuelewa Morrison kama badala ya kumkanyaga tumboni Mwaikenda angemkandika ngumi ya Uso Arajiga aliyemwacha Sospeter Bajana akitamba wakati alistahili Kadi nyekundu Tangu kipindi cha Kwanza.
Leo ukisoma comments za wachambuzi mitandaoni Kila mmoja anatetea upande anaoupenda. Mmoja amefikia kumuona Bajana shujaa, mwingine anasema Morrison alifanya vile Kwa sababu Yanga wamekuwa wakikanyagwa bila Waamuzi kuchukua hatua Kwa hiyo na wao wameamua kurevenge. Maoni ya kitoto yanayotolewa na watu wazima wanopaswa kuona uchungu Wachezaji wanapoumizwa.
Naaasihi wachambuzi wa nchi hii, kuna vingi vya kuchambua. Kama mnaona soka si saizi yenu chambueni hata mchezo wa bao ambako Wachezaji hawaumizani, wanakula nyumba na kulala nje.