Mnaojiita Wachambuzi wa Soka Tanzania ni Bora mjiite mashabiki kuliko kudanganya Umma

Bila bila

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2016
Posts
22,168
Reaction score
39,118
Jana kulikuwa na Mechi iliyobayizwa jina la Derby ya Dar es salaam Kati ya Yanga na Azam iliyomalizika Kwa matokeo ya 2-2. Kama ilivyo kawaida ya Mechi ngumu haikosi matukio. Kinachotrend Kwa Sasa zaidi ya matokeo ni maamuzi ya mwamuzi wa Mechi ya Jana katika baadhi ya matukio aliyopaswa kuamua vinginevyo.

Kwa Leo hiyo si hoja yangu. Hoja yangu ni jinsi wanaoitwa wachambuzi wa soka àmbao Kwa nchi nyingine watu wanawategemea kusikia maoni yaliyoshiba wanavyobebwa na ushabiki na kuchambua Kwa uelekeo wa mapenzi Kwa timu.

Nikichukua Mechi 3 zilizozua mijadala zaidi nchini ikiwemo ya Jana nawaona wachambuzi kama wachochezi katika matukio badala ya kukosoa Kwa Nia ya kujenga.

1.Coast Union Vs Yanga tukio la faulo ya Mtenje Jr dhidi ya Bangala halikupaswa kuwagawanya wachambuzi wakawepo wa kulaani tukio na mwamuzi Kwa kutochukua hatua sitahiki na wale wanaotetea tukio lile eti rafu ni sehemu ya mchezo na maamuzi ya refa ni madhaifu ya kibinadamu. Kesho Mtenje atafanya tena Kwa vile alipata watetezi, itamgharimu yeye na timu yake akichukuliwa hatua sitahiki na itamgharimu mchezaji atakayeumizwa na inaweza kuwa mwisho wa maisha yake kisoka tukapoteza kipaji.

2.Yanga Vs Simba Ngao ya hisani limejadiliwa Sana tukio la Inongà dhidi ya Salim Abubakar. Eti nalo lilipata watetezi kwamba Kwa vile Salim alimkwepa na kisha kureact basi refa alitumia busara. Ni kweli hakimu apaswa kuwa na busara, lakini kutoa hukumu ya haki ni busara pia. Hata kama angemtoa na Salim Abubakar bado ingekuwa busara na ingewaonya wote wawili wasirudie waliyoyafanya.

3.Komesha ni Jana Yanga Vs Azam
Wapo na hata Kwa majina wamejiandika wanaoona "busara" ya Refa Kwa kitendo cha rafu mbaya ya Bajana dhidi ya Job iliyopelekea kutoendelea na mchezo ni Jambo zuri. Lakini Huyo Huyo anayeona Bajana ambaye hakuadhibiwa ipasavyo na ikampa kichwa akamfanyia rafu nyingine mbaya Bernard Morrison, ndio wanaoona refa hakutenda busara kutomwonyesha Kadi nyekundu mchezaji aliyefanya Upumbavu na unyama uliopitiliza Bernard Morrison dhidi ya Lusajo Mwaikenda. Hakuna busara njema ya kuacha mhalifu aendelee bila adhabu.

Kitendo cha Bajana na Morrison kumaliza salama Mechi ya Jana kwangu ni doa kubwa Kwa mwamuzi. Huwezi kuwa na Wachezaji wanaofikiria kuumiza wenzao uwanjani wakati wao wakiumizwa wanalalamika. Ningemuelewa Morrison kama badala ya kumkanyaga tumboni Mwaikenda angemkandika ngumi ya Uso Arajiga aliyemwacha Sospeter Bajana akitamba wakati alistahili Kadi nyekundu Tangu kipindi cha Kwanza.

Leo ukisoma comments za wachambuzi mitandaoni Kila mmoja anatetea upande anaoupenda. Mmoja amefikia kumuona Bajana shujaa, mwingine anasema Morrison alifanya vile Kwa sababu Yanga wamekuwa wakikanyagwa bila Waamuzi kuchukua hatua Kwa hiyo na wao wameamua kurevenge. Maoni ya kitoto yanayotolewa na watu wazima wanopaswa kuona uchungu Wachezaji wanapoumizwa.

Naaasihi wachambuzi wa nchi hii, kuna vingi vya kuchambua. Kama mnaona soka si saizi yenu chambueni hata mchezo wa bao ambako Wachezaji hawaumizani, wanakula nyumba na kulala nje.
 
Uchambuzi wa mpira (michezo) ni maoni binafsi ya mtu kama vile nawe umetoa maoni yako kutokana na mchezo husika. Yeye(wao) kaona/wameona hivyo una hiari kukubaliana nao au kutokubaliana nao. Cha msingi hapa ni nawe kutoa maoni yako, na usifikiri ndio 100% yako sahihi, kuna wataokuunga mkono na wataokuona umetoa pumba. Wote mko sahihi kwani haya ni maoni binafsi.

Kuna Thread kama hii huko nyuma, mtoa thread alishauri hao wachambuzi waende shule. Ukweli ni kwamba hakuna shule ya wachambuzi, bali wachambuzi wengi wa nchini na kimataifa huwa aidha:
  1. Wachezaji wa ngazi ya juu(Taifa) wa muda mrefu waliostaafu hivyo wanauzoefu wa kutosha wa mchezo husika
  2. Makocha wa kiwango hicho/ mfano wa Simba, yanga, Azam , Taifa stars n.k
  3. Watangazaji wa michezo wa muda mrefu
Hivyo ndivyo utawakuta wachambuzi wa kimataifa walvyo.
Nayo ni maoni yao tu.
 
Jana kulikuwa na Mechi iliyobayizwa jina la Derby ya Dar es salaam Kati ya Yanga na Azam iliyomalizika Kwa matokeo ya 2-2. Kama ilivyo kawaida ya Mechi ngumu haikosi matukio. Kinachotrend Kwa Sasa zaidi ya matokeo ni maamuzi ya mwamuzi ...
Mpira wa Simba na Yanga Tanzania ni takataka tuliyoamua wenyewe tukae nayo, awe kiongozi awe shabiki au hata hao wachambuzi hufanya mambo yao kwa kuangalia timu hizo mbili

Mi kila siku naombea hizo timu mbili zishuke daraja zikae nje ya ligi kwa miaka kadhaa kutokea hapo ndio tutapata maendeleo ya soka tofauti na hapo nchi zote zilizokuwa chini yetu zitaendelea kutukanyaga ona Uganda wanavyotufanyia kila mara
 
Wachambuzi wote duniani ni bendela fata upepo.

Timu ikishinda husikii wakisema udhaifu wake lakin udhaifu unakuwepo siku ikifungwa unasikia sasa wanavyoichambua sjui huwa haiko vizur sjui wapi na wapi inatakiwa wafanye usajir wa nani na nani
 
Wachambuzi wote duniani ni bendela fata upepo.

Timu ikishinda husikii wakisema udhaifu wake lakin udhaifu unakuwepo siku ikifungwa unasikia sasa wanavyoichambua sjui huwa haiko vizur sjui wapi na wapi inatakiwa wafanye usajir wa nani na nani
 
Wachambuzi nao wana mapenzi na hizi timu mbili kama ilivyo wewe, yes sijakosea nasema tena kama ilivyo wewe kuwa na mapenzi na Club yako
 
Shida ulitaka achambue kama unavyotaka wewe... Mwandiko wako unaonesha wewe ni da ya afrika
 
Kuja kulalamika humu wakati bado unaendelea kuwafollow na kuwafatilia nao ni aina fulani ya ujuha
 
Huwa nakerwa sana na wachezaji wanaocheza faulo mbaya, hatarishi na za makusudi kabisa wakati wa mchezo! halafu mwamuzi hachukui hatua stahiki.

Huu ni udhaifu mkubwa sana kwa waamuzi wetu.
 
Hasa kajamaa kanajiita Privalidinho, sijui kama hata mpira kanaujua vizur na sheria zake
 
Ndio haohao wanaotoa hoja kwamba wachezaji wetu wengi sio bora kwa kuwa hawajapitia katika misingi bora ya soka lakini wanaamini kuwa kwa kutumia mashindano mbalimbali ya mitaani wanayoyaandaa yataibua wachezaji bora watakaokuwa msaada kwa vilabu na nchi!!!
 
Huoni aibu utopolo
 
Tanzania hakuna wachambuzi bro!wasikuumize kichwa kabisaa!wazushi tu hawaa!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…