Mnaojua mpira vizuri msipoteze muda wenu kwenda Taifa leo bali nendeni kwa wingi Kesho

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Nitawadharau na kuwapuuza mno Watu ambao wanajiita ni wa Mpira halafu leo wakapoteza kabisa muda wao kwenda Uwanja wa Taifa kutizama mechi ya Kombe la Klabu Bingwa Afrika baina ya Yanga SC ya Tanzania dhidi ya St. Louis ya Shelisheli wakati tayari matokeo tunaojua mpira tumeshayajua kwamba leo Yanga SC itashinda kati ya Goli Saba ( 7 ) hadi Tisa ( 9 ) na ikiwezekana hata Goli Kumi ( 10 ) na kwamba utakuwa ni mchezo wa upande mmoja tu.

Ukitaka kutizama mpira bora na kuburudika ili hata usiboreke na kujutia kupoteza Pesa yako basi ni matumaini yangu makubwa wale Wenzangu tunaojua mpira ( Wadau wakubwa wa Soka la Bongo / Tanzania ) Kesho tutajazana na kujitokeza kwa wingi wetu kabisa kwenda kuitizama mechi ambayo nina uhakika itakuwa nzuri na yenye mvuto wote kati ya Simba SC ya Tanzania dhidi ya Gendamarie FC ya Djibouti.

Mnaopanga kwenda Taifa leo nawashauri okoeni Pesa zenu ili mkaitizame Simba SC Kesho Taifa.

Nawasilisha.
 
Umetumwa na Haji ?
 
Djibouti tangu lini ikawa nchi ya mpira?

Round hii Simba na Yanga zote zinavuka tusubili round ijayo Yanga inatupwa Misri na Simba inatupwa Nigeria mchezo umekwisha tunarudi kwenye ligi yetu ya maharage.
 
mbona Yanga haijafunga hizo goli 9 ?. sie wanazi wa simba tulilazimika kuishangilia sana Yanga leo hadi wakapata goli la ushindi. hongereni sana Yanga
 
Kunawatu wana fikira mgando sana kama jiwe yani au zindiko sasa magoli hayo saba yakowapi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…