Mnaokopa kwenye mitandao ya simu na kubadili laini ili kukwepa mikopo, BOT watoa muongozo

Mnaokopa kwenye mitandao ya simu na kubadili laini ili kukwepa mikopo, BOT watoa muongozo

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Wakuu,

Imeelezwa watu wenye tabia ya kukopa mikopo ya mitandaoni na kisha kubadili laini zao za simu ili kukwepa ulipaji wa mikopo hiyo wapo hatarini kukosa mikopo kutoka kwenye taasisi zingine za fedha zinazotambulika kisheria.

Hiyo ni kutokana na kuwepo kwa kanzidata ya kumbukumbu ya madeni ya wateja wote wanaokopa kwenye mitandao.

Kauli hiyo imetolewa Februari 25,2025 na Afisa kutoka Kurugenzi ya Tafiti na Sera za Uchumi wa BOT,Dominic Mwita wakati akiwasilisha mada ya mfumo wa utekelezaji wa sera ya fedha kwa njia ya riba iliyoanza Januari 2024 katika semina ya waandiishi wa habari inayofanyika Mkoani Mtwara.

Mwita amesema wakati mwingine mtu anaweza kutaka kumtumia mtu mwingine fedha kiasi cha shilingi 500 alafu amepungukiwa shilingi 50 ,mtandao wa simu unaweza ukakukopesha na inapopita kadhaa tofauti na makubaliano ya kukukopesha hujalipa basi , taraifa zako zinapelekwa kwenye kanzidata kwamba ni mdaiwa sugu asiyelipa mkopo wake.

Ametoa wito kwa jamii pindi mtu anapokopa wajibike kulipa deni lake hata kama ni fedha ndogo na si kubadilisha laini kwani kwa kufanya hivyo kunaendelea kumuweka kwenye hatari ya kutoaminika tena na hivyo kutokopesheka tena hata kwenye mitandao mingine na taasisi zingine za fedha.

botttt.png
 
Daah Huko kwa mitandao wanakopa kiasi gani?, wakopaji ni wanafunzi wa vyuo u?, Bongo nyoso.
 
Back
Top Bottom